MFUASI MTATA WA CHADEMA HUKO FACEBOOK AMUIBUKIA MSANII CHID BENZ ALIYEMTUKANA LOWASSA ONA LIVE!!
WASANII WASIPOJIFUNZA KWA CHIDI NDIO BASI TENA.!
By Malisa GJ.!
Sikutaka kuandika chochote leo kwny ukurasa huu baada ya kudedicate kwa mwanadada mtanzania aliyebuni sofware yake Leah-Buzuka. Lakini nimelazimika kuandika kutokana na mshtuko nilioupata baada ya kumuona Msanii wa muziki wa Bongofleva Chid Benz katika hali ya kutia simanzi.
Kwa ujumla Chid Anaumwa na anahitaji msaada. Hajasema hasa anaumwa nini ila inadaiwa ni athari za madawa ya kulevya.
Lakini maisha ya Chid yamenifanya nitafakari sana juu ya "nini maana hasa ya maisha?".. Nimeumia kumuona kijana mwenzangu ambaye alishaanza kung'aa katika sanaa kuwa katika hali hii.
Nakumbuka wakati Chid akiwa kwenye "peak ya mafanikio" alikua na mashabiki na wapambe wengi. Alipata mafanikio mazuri kimuziki. Nakumbuka alikua na kipindi EATV kikizungumzia maisha yake nje ya muziki.
Kilikua ni kipindi kizuri ambacho kingempa opportunity ya kufanya biashara na wadau mbalimbali kama angeweza kutumia fursa hiyo vizuri. Kupitia kipindi hicho Chidi angeweza kuingia mikataba ya matangazo na makampuni mbalimbali na akaongeza kipato.
Lakini nasikia alishindwa kumaintain kutokana na kutumia sn madawa ya kulevya hali iliyopelekea kunyang'anywa hiyo "air time". Kama Chid angekua na nidhamu ya kazi leo angekua level za kina Diamond, Ila kwa sasa ni mgonjwa, kadhoofika mno ma anahitaji msaada kwa wasamaria wema.
Maisha yanatupa funzo kubwa kuwa hujafa hujaumbika. Ukiwa na nafasi leo itumie vzr na usimdharau yule asiyekuwa nayo. Historia ya Chid inatupa mengi ya kujifunza.
#September_20_mwaka_2015 Chid alitoa wimbo wimbo wake unaoitwa "makavu kwa Lowassa na Chadema". Wimbo huu una matusi mazito ya nguoni kumhusu mgombea Urais wa UKAWA Mhe.Edward Lowassa na CHADEMA kwa ujumla.
Wimbo huu ulikua uploaded kwenye Youtube tar 25 September 2015 na Wema Sepetu. (Ingia Youtube andika matusi kwa Lowassa au click hii adress uusikilize moja kwa mojahttps://m.youtube.com/watch?v=r-mG5ftslFo).
Sehemu ya Maneno kwenye wimbo huo Chid anasema "ukiwa mwizi uraiani huwezi kuacha wizi ukienda ikulu, ukiwa mgonjwa uraiani huwezi kupona ukienda Ikulu"
Hapa Chid alikua akiendeleza ile propaganda ya CCM kwamba UKAWA wana mgombea mgonjwa. Sasa najaribu kumuangalia Lowassa alivyo sasa na Chid alivyo sasa najiuliza nani mgonjwa kati yao? Je Chid alimtukana Lowassa kwa utashi wake? Kama sio utashi wake alitumwa na nani? Ka ujira gani? Mbona huyo aliyemtuma akaponde afya ya Lowassa hakumsaidia Chid kuimarisha afya yake kwanza?
#March_22_mwaka_2013,
Chid wakati huo akiwa na nguvu nyingi na afya nzuri alimpiga msanii mwenzake Marehemu "Mangwair" katika ukumbi wa "Ammbassador Loungue" uliopo kwny jengo la Benjamin Mkapa Tower jijini Dar. Sina hakika kama Chid aliweza kumuomba Ngwair msamaha kabla ya kifo chake.
#June_20_mwaka_2012
Chid Benz akiwa bado na afya nzuri alimtukana msanii mwenzie Profesa Jay na kutaka kumpiga ktk ukumbi wa Dar-West Park Tabata, kabla hawajaamuliwa na mashabiki.
Sababu ya kufanya hivyo Chid alidai ni Prof.Jay kusema ktk kipindi cha "Mkasi cha EATV" kwamba yeye ndio alimuibua Chid na alimuombea ruhusa kwa mama yake ili amruhusu Chid kufanya muziki. Chid akakasirishwa na maneno hayo na kutaka kumfanyia fujo Proffessor Jay. Sina hakika kama Prof.Jay alisema maneno hayo au Labda Chid alikua anatafuta tu sababu ya kumfanyia fujo maana alishazoea fujo.
Lakini hata kama Prof.Jay hakusema, je ukweli ni upi? Ukweli ni kwamba Prof.Jay ndiye aliyemuibua Chid. Hata jina "Chid Benz" alipewa na Jay. Wakati Chid anaanza muziki alikua anajiita "Benzino" jina la msanii wa Marekani. Professor Jay akamshauri atafute identity yake. Huwezi kuwa msanii mkubwa kwa kutumia jina la msanii mwingine. Hivyo akabadili na kujiita "Chidi" kama kifupisho cha jina lake Rashid Abdala Makwiro. Professor Jay akamsaidia kuunganisha jina "Chid" ambalo ni kifupi cha "Rashid" na jina "Benz" ambalo ni kifupi cha "Benzino", hivyo akapata "brand name" yake "Chid Benz" ambayo anaitumia hadi leo.
Najaribu kujiuliza hivi Chid angeambiwa anaweza kuwa ktk hali hii aliyonayo leo halafu yule aliyetaka kumpiga (Prof.Jay) akawa Mbunge angeamini? Anyway maisha ni safari yenye mafunzo mengi njiani.
#May_05_mwaka_2013
Chidi alijaribu kumfanyia fujo msanii mwenzie wa BongoFleva "KalaPina" kwa kuvamia steji katika ukumbi wa Maisha Club Msasani. Lakini Kalapina alimdhibiti na Chid akaishia kupigwa yeye. Kala Pina alimwambia "usidhani mimi ni Ngwair"
#January_05_mwaka_2015
Chidi alimpiga mwandishi mmoja wa habari (jina nalihifadhi) kwa madai kuwa alimripoti vibaya alipokamatwa na madawa ya kulevya. Inadaiwa alimtwanga mwandishi huyo kabla "Babu Tale" kuingilia kati na kumuokoa.
Ripoti ya matukio ya utukutu ya Chid ni ndefu sana na pengine tunaweza kuelezea orodha ya matukio yake bila kumaliza maana ni ndefu sana.
Lakini kwanini Chid alikua mtukutu kwa kiwango hiki? Je ni sababu ya nguvu alizokua nazo? Je ni kiburi, ubabe, majivuno, fedha au wapambe? Je hakuwahi kufikiri kuwa siku moja anaweza kudhoofu na akashindwa kumpiga hata mtoto mdogo licha ya watu wazima aliokuwa akiwapiga?.
Chidi amedhoofika kabisa kiafya kwa kile kinachodaiwa ni athari za madawa ya kulevya. Chid amechoka sana. Madawa yamemmaliza kabisa.
Lakini hili si tukio la kwanza kwa wasanii wa bongo kuumizwa na madawa ya kulevya. Wapo wengi na wengine wameshakufa sababu ya "drugs" lakini hawajifunzi. Msanii "Langa" aliathiriwa sana na madawa ya kulevya. Alifanikiwa kuacha na akawa "agent" wa kushawishi wengine waache lakini hadi umauti unamfika alikua bado amedhoofu sana kimwili kutokana na athari za madawa ya kulevya.
"Ray C" nae aliathiriwa sana na madawa ya kulevya na kama si juhudi za Rais Kikwete kumsaidia pengine tungekua tunaongea mengine hivi sasa.
Lakini je wasanii wanajifunza? Na sisi tusio wasani maisha yanatupa somo gani? Binafsi nimefunza kuwa miili tuliyonayo ni ya thamani sana. Ni mahali pekee ambapo unaweza kuishi. Mwanafalsafa Jim Rohn aliwahi kusema "take care of your body because it's the only place you can live in" Akimaanisha "utunze sana mwili wako maana ni mahali pekee unapoweza kuishi".
Bila hii miili hatuwezi kufanya lolote, hatuwezi kuishi. Kwa hiyo ni vizuri tukaitunza vizuri. Tusiitese kwa madawa ya kulevya, pombe, zinaa au mambo mengine yanayoweza kuhatarisha afya zetu. Afya yako ni ya thamani sana kuliko kitu kingine chochote duniani.
Mwanasayansi aliyebuni computer za Apple Bw.Steve Jobs ktk dakika za mwisho za uhai wake alisema "I reached the pinnacle of success in the bussiness world, but aside from work I have a little joy... at this moment, lying on the sick bed and recalling my whole life, I realize that all the recognition and wealth that I took so much pride in, have paled and become meaningless in the face of impending death"
Akimaanizha kuwa licha ya kufanikiwa sn kibiashara lakini maisha yake hayakua na furaha. Alipolala ktk kitanda cha wagonjwa na kufikiria maisha yake yote aliyoishi duniani, aligundua kwamba utajiri wote aliokua nao hauna maana mbele ya mauti.
Kwa Steve Jobs afya yake ilikua ya muhimu kuliko utajiri wote aliokua nao. Lakini utajiri wa Steve Jobs haukumsaidia kitu mbele ya mauti. Alikufa na kuacha utajiri wote wa mabilioni ya dola. Usipokuwa na afya nzuri vyote ulivyonavyo ni kazi bure.
Nitumie fursa hii kuwaasa wasanii wa bongo waache kuumiza afya zao kwa madawa ya kulevya. Hata kama wanapata fedha lakini fedha hizo hazina maana kama mwisho wake ni kama huu wa Chid Benz. Kama hutaki kujifikiria wewe, Kumbuka kuna watu nyuma yako. Kumbuka ndugu zako, mke wako, watoto, marafiki, jamaa zako wataumia kiasi gani.
Nimesikitika kumsikia Chid akisema mama yake analia kila siku kumuona katika hali hiyo. Anamwambia "wale marafiki zako ulipokua unaimba wako wapi? Watafute wakusaidie."
Chid aliposema maneno ya mama yake nikakumbuka kauli ya rafiki yangu mmoja alipata kuniambia "ukiwa na mafanikio dunia nzima inakukimbilia, lakini ukiwa na matatizo dunia nzima inakukimbia. Unabaki peke yako na kimbilio lako la mwisho ni familia"
Familia ndio hubeba mzigo wote wa negative impacts. Mhanga mkuu wa maisha yako ya duniani ni familia. Ukifukuzwa kazi kimbilio lako la kukufariji ni familia. Ukifukuzwa shule wanaohangaika na wewe ni familia. We pata pesa kula bata na washkaji lakini ukiugua familia yako ndiyo itaugua na wewe.
Mama yako ndiye atayateseka, baba yako ndiye atakayekua rafiki yako wa karibu maana marafiki hutawaona, mke/mume wako ndiye atakuogesha na kukulisha. Ukiwa ktk dhiki kuu kimbilio la mwisho huwa ni familia. Ipende familia yako, ijali, ihudumie vzr. Kipaumbele cha kwanza ktk maisha yako kiwe familia yako. Hao wengine wafuate baadae. Naipa pole sana familia ya Chid Benz. Nampa pole mama yake Chid. Najua ni uchungu kiasi gani anaoupata kumuona mwanae katika hali hii. Namuombea Mungu ampe uvumilivu ktk kipindi hiki kigumu.
Namuombea pia Chid aweze kupona na kurudi katika afya yake. Namuombea msaada kwa watanzania watakaoguswa wawasiliana nae kuona namna ya kumsaidia. Mwisho nawaomba wasanii na watanzania kwa ujumla wajifunze kwa Chid. Dawa za kulevya zina athari mbaya sana. Tusingoje kuwa mfano kwa wengine.
Malisa GJ
No comments: