MAHUSIANO Mambo Matano ya Uongo Unayopaswa Kuacha Kuyaamini Kuhusu Tendo la Ndoa





Kuna mambo mengi ya uongo yanayoaminika na watu wengi kuhusu tendo la ndoa, mambo ambayo yanaweza kuhatarisha usalama wa penzi 
lako.
YAFUATAYO NI MAMBO MATANO YA UONGOUNAYOPASWA KUACHA KUYAAMINI KUHUSU TENDO LA NDOA;
Tendo la ndoa lazima liwe sahihi
Katika hali ya kawaida watu wengi katika mahusiano hujiwekea shinikizo binafsi la kuwa, ni lazima tendo la ndoa lifanywe katika usahihi. Huwezi kumfikisha mpenzi wako kileleni kama unafanya tendo la ndoa hali ukiwa na wasiwasi wa ufanisi wako. Ikumbukwe kwamba ukitaka kulifurahia tendo la ndoa pamoja na mpenzi wako mnapaswa kuweka nia katika raha ya tendo kuliko usahihi wa tendo.
Tendo la ndoa lifanywe kwa uhiari na sio kwa kupangwa
Je, kweli utarajie tendo la ndoa kuwa tendo la hiari hata baada ya kuwa katika mahusiano kwa muda mrefu? Achana na imani potofu ya kuwa, kuweka mipango maalum ya kufanya tendo la ndoa na mpenzi wako inamaanisha kuwa hauna mapenzi ya dhati na mume au mke wako. Unashauliwa kuweka mipango maalum ya kufanya tendo la ndoa na mpenzi wako hasa kama unataka kujijengea maisha bora ya tendo la ndoa.
Wanaume wanapenda kushiriki tendo la ndoa kila mara
Jinsia ya kiume imekuwa ikiandamwa na kashfa hii mbele jamii na tafiti mbalimbali kuwa ndiyo jinsia pekee inayopenda kushiriki tendo la ndoa kila mara. Jambo ambalo si kweli. Kwani kama ilivyo kwa upande wa wanawake kuwa na muda ambao hawajisikii kufanya tendo la ndoa, ndivyo ilivyo  kwa upande wa wanaume pia. Kuna muda fulani mwanaume atakuwa katika kilele cha juu cha hamu ya tendo na kuna muda mwingine atakuwa katika kilele cha chini cha hamu ya tendo. Kwa msaada zaidi soma Makala hii Mabadiliko ya Hamu ya Kufanya Tendo la ndoa kwa Mwanaume na Mwanamke Katika Mzunguko wa Masaa 24
Wanawake wanapaswa kufikishwa kileleni daima
Si jambo la busara mwanamke kujiwekea shinikizo binafsi la kutaka kufika kileleni kila mara unaposhiriki tendo la ndoa kwa kuwa zipo sababu mbalimbali zinazoweza kuzuia hilo, ikiwemo hali ya kawaida kabisa ya wanawake kuchelewa kufika kileleni ukilinganisha na wanaume. Hivyo ni bora kuwa mvumilivu na kuwa mtu wa kutafuta suluhu ya matatizo kama hilo hasa linapokuwa la kudumu. Unaweza pia kusoma hii kwa msaada zaidi Tendo la Ndoa: Mkeo Anakosa Hamu Ya Tendo La Ndoa? Msaidie Hivi
Tendo la ndoa lina ladha mnapokuwa vijana
Watu wengi wanaamini kuwa tendo la ndoa lina ladha tu pindi wapenzi wanapokuwa vijana, na hivyo huacha kuendelea kulifurahia wanapofikia umri mkubwa. Utafiti wa mwaka 2015 uligundua kuwa karibu asilimia 54% ya wanaume na asilimia 31% ya wanawake wenye umri kati ya miaka 70 na 80 hushiriki tendo la ndoa angalau mara mbili kwa mwezi .



No comments:

Powered by Blogger.