Idris Aeleza Matumizi ya Milioni 500 za Big Brother Baada ya Kuambiwa Amefilisika
Mshindi wa Big Brother Africa 2014, Idris Sultan aeleza jinsi alivyozitumia milioni 500 za Big Brother baada ya watu kwenye mitandao ya kijamii kudai amefilisika.
Akizungumza katika kipindi cha Friday Night Live cha East Africa Television Ijumaa hii, Idris alisema pesa yote aliyoshinda imeishia kwenye miradi mbalimbali.
“Pesa yote milioni 500 niliyoipata kwenye Big Brother Africa imeisha!!. Imeisha kwa sababu ya investment, nimeinvest sana,” alisema Idris.
Mwishoni mwa mwaka jana, Idris alitangaza ujio wa vipindi vyake viwili vya TV ambavyo vitarushwa kupitia vituo vya runinga vya Vuzu, Afrika Kusini na BET Africa pia aliwahi kuweka wazi kuwa anamiliki kampuni ya matangazo.
Jiunge na Bongo5.com sasa
No comments: