Eti hii ndio itakuwa mechi yake ya kwanza Pep Guardiola atakapojiunga na Man City
Kocha wa zamani wa klabu ya FC Barcelona ya Hispania ambaye kwa sasa anaifundisha klabu ya FC Bayern Munich
akimalizia mkataba wake, kabla ya
kujiunga naMan City mwishoni mwa msimu Pepe Guardiola, tayari mechi
yake ya kwanza akijiunga na Man
City kuna tetesi
kuwa imejulikana.
Pepe Guardiola anatajwa kuwa na
tetesi mechi yake ya kwanza itakuwa dhidi ya Man
United ambayo
inadaiwa kuwa kwa wakati huo itakuwa ikifundishwa na Jose Mourinho, ila itakuwa ni
michuano ya maandalizi ya msimu ‘International
Champions Cup’itakayofanyika Beijing
China.
Hata hivyo ukweli wa kukutana au kutokukutana
utajulikana wiki hii, kwa sasa mashabiki wa Man
United wanaimani
kuwa Louis
van Gaal atafukuzwa
mwishoni mwa msimu naMourinho atajiunga nao, wakati Man City wao walithibitisha kuwa tayari
walisaini mkataba na Guardiola.
No comments: