Utafiti: Umaarufu Wa Lowassa Waporomoka, Magufuli Apaa

Matokeo ya utafiti mpya
uliofanywa mapema mwezi huu yanaonyesha kuwa umaarufu
wa Rais John Magufuli
umeongezeka kufikia asilimia 74.5, akimuacha mbali mpinzani wake wa karibu
kwenye Uchaguzi Mkuu, Edward Lowassa.
Magufuli alishinda mbio
za urais kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, akipata asilimia chache kuliko
wagombea wengine kutoka CCM, lakini amejiongezea umaarufu kutokana na hatua
ambazo amekuwa akichukua tangu alipoapishwa Novemba 5, 2015.
Katika uchaguzi huo, Dk
Magufuli alipata kura milioni 8.8 sawa na asilimia 58.47, akifuatiwa na Lowassa
aliyepata kura milioni 6.07, sawa na asilimia 39.97.
Lakini utafiti huo
uliofanywa na taasisi ya Ms Infotrak Researc and Consultant na Ms Midas Touche
East Africa kwa kuwahoji watu 1,200 wenye umri wa zaidi ya miaka 18 katika
kanda sita na mikoa 15, unaonyesha kuwa Magufuli ameongeza umaarufu kwa
takriban asilimia 20, huku Lowassa akishuka kwa asilimia 20 pia.
Katika utafiti huo,
Lowassa anaonekana kushuka hadi asilimia 20.1.
Wengine waliotajwa
katika orodha hiyo ni Anna Mghwira aliyepata asilimia 1.1, Hashimu Rungwe
(0.4), Fahmi Dovutwa (0.2), Lutalosa Yemba (0.1), Janken Kasambala (0.1) na
Machmillan Lyimo aliyepata asilimia 0.0. Asilimia 3.5 ya walioulizwa swali hilo
walikataa kujibu.
Vilevile, wananchi
walipouliza iwapo Uchaguzi Mkuu ukifanyika leo wangemchagua nani kati ya makada
waliojitokea kugombea urais mwaka jana, wengi wamemtaja Magufuli.
Matokeo hayo yanaonyesha
kwamba wanawake wengi ndiyo wanamuunga mkono Magufuli ikilinganishwa na
wanaume.
Asilimia 77.9 ya
wanawake wanasema wapo tayari kumchagua tena kuwa Rais iwapo kutakuwa na
uchaguzi mpya, wakati wanaume wanaosema hivyo ni asilimia 71.5 pekee.
Kinyume na ilivyo kwa
Magufuli, utafiti umebaini kwamba Lowassa anapendwa zaidi na wanaume huku
asilimia 22.6 wakisema wapo tayari kumchagua kuwa rais. Ni asilimia 17.4 ndiyo
wametoa maoni kama hayo kwa Magufuli.
Kwa upande wa kanda;
Kanda ya Zanzibar ndiyo inayoongoza kwa ‘kumkubali’ Magufuli ikiwa na asilimia
91.6, ikifuatiwa na Kanda ya Kati yenye asilimia 81.6, Kanda ya Kaskazini
(77%), Kanda ya Pwani (72.7) na Kanda ya Ziwa asilimia 67.6.
Alipoulizwa kuhusu
matokeo ya utafiti huo, mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Profesa George
Shumbuso alisema kuongezeka kwa umaarufu wa Rais Magufuli kunatokana na
utendaji wake kugusa kero za wanyonge.
Alisema Watanzania wengi
hata wale waliokuwa wakiunga mkono vyama vya upinzani, wameanza kukubaliana na
Magufuli kutokana na namna alivyoweza kufanya mambo makubwa na yenye umuhimu
kwa Taifa ndani ya muda mfupi.
“Hakuna Rais aliyefanya
mambo makubwa namna hii ndani ya siku 100 ndiyo maana wanyonge wameonekana
kumkubali kwa sababu amegusa na kuonyesha wazi nia ya kumaliza changamoto zao,”
alisema.
“Hata ikitokea uchaguzi
ukafanyika sasa nina uhakika Magufuli atashinda kwa sababu wananchi wamebaini
wazi kuwa anachokizungumza ndicho anachomaanisha. Si siasa kama ambavyo
imezoeleka kwa wanasiasa wengine.”
Kauli hiyo iliungwa
mkono na mwenyekiti wa Tanzania Labour Party na mbunge wa zamani wa Vunjo,
Augustine Mrema aliyesema kuwa Watanzania walifanya uchaguzi sahihi kumuweka
Magufuli madarakani.
Alisema katika kipindi
cha siku 100 kiongozi huyo amefanya miujiza ambayo hakuna Mtanzania ambaye
alifikiria kuwa ingeweza kufanyika
No comments: