Unaambiwa Magufuli Kuzuia Safari za Nje Kwa Vigogo Imeokoa Mabilioni ya Pesa...
Badala ya sherehe za
Uhuru, tumefanya usafi ili kupambana na
kipindupindu, na fedha zilizookolewa
zinajenga sehemu ya barabara iliyokuwa kero kubwa kwa wananchi.
Badala ya Rais na
Wabunge kujipongeza kwa sherehe kubwa, fedha zilizookolewa zimetatua tatizo la
vitanda kwa wagonjwa.
Badala ya sherehe za
siku ya UKIMWI, fedha zimekwenda kununua dawa za kufubaisha makali ya UKIMWI.
Badala ya semina elekezi
ya Mawaziri, fedha zake zitakwenda kutekeleza mradi wa kufunga vifaa vya kisasa
vya kuchunguza magonjwa katika hospitali 37 kote nchini.
Badala ya safari za nje
fedha zilizookolewa zitatumika kwenye miradi ya maendeleo. Zaidi ya
Sh.7 bilioni ambazo zingeweza kutumika kwa safari za nje zimeokolewa katika
siku 100 na zitatumika kwenye miradi hiyo ya maendeleo.
Hatua hizo, na nyingine
nyingi, zimevuta hisia za watu mbalimbali kote duniani. Mnaofuatilia mitandao
ya kijamii mnajua hivyo, na wapo wameonesha wazi kutamani tungewaazima Rais
wetu kwa muda" Alisema Balozi Ombeni Wakati akitoa Tasmini ya Siku 100 za
Rais Ikulu

No comments: