Tazama goli la kwanza la Samatta lililoipa point tatu muhimu KRC Genk dhidi ya vinara wa Ligi leo
Jumapili
ya February 28 Ligi Kuu Ubelgiji
iliendelea tena kwa klabu ya KRC
Genkinayochezewa na mtanzania Mbwana Samatta kushuka katika uwanja wake wa
nyumbani Cristal Arena kucheza mchezo wake wa 28 wa Ligi Kuu
dhidi ya vinara wa Ligi Club Brugge.
Licha ya
kuwa Club Brugge walikuwa wanarekodi nzuri dhidi ya Genk wamekubali kipigo cha goli 3-2, kwani
kabla ya mchezo huo, Genk na Brugge kwa mechi tano zilizopita,Brugge walikuwa wameifunga Genk mara tatu, sare moja na kupoteza mechi
moja.
Magoli
ya KRC Genk yalifungwa na Nikolaos
Karelis dakika ya
31, ikiwa ni dakika 21 zimepita toka Club Brugge wapate goli la kuongoza dakika ya 15
kupitia kwa Thomas Meunier,
lakini kasi ya Genk iliongezeka na kupata goli la pili
dakika ya 50 kupitia kwaThomas
Buffel.
Mbwana
Samatta aliingia dakika ya 79 kuchukua
nafasi ya Nikolaos Karelis aliyefunga goli la kwanza la KRC
Genk. mabadiliko ya kuingia Mbwana Samatta yalikuwa na faida kwani, dakika 2
baada ya kuingia alipachika goli lake la kwanza akiwa na Genk lakini pia ni goli la tatu kwa Genk,
kabla ya dakika ya 83 Brugge walifanikiwa kupata goli la pili.
No comments: