Refarii apigwa risasi na mchezaji Argentina
Refarii mmoja nchini Argentina amepigwa risasi na kuuawa na mchezaji
aliyemuonesha kadi nyekundu uwanjani katika mechi ya daraja la pili.
Refarii huyo Cesar
Flores alikuwa akisimamia mechi baina ya timu zinazoshiriki ligi ya daraja la
chini mjini Cordoba, takriban kilomita 700 Kaskazini mwa Buenos Aires.
Polisi wameanzisha
msako mkali kumtafuta mchezaji huyo ambaye hadi sasa hajatajwa.
Refarii Flores
alimuonesha kadi nyekundu mchezaji huyo na akaondoka uwanjani kama ilivyo ada.
Lakini baada ya
kipindi fulani alirejea akiwa amefoka uwanjani na kumfyatulia refarii huyo
risasi 3 ; Kifuani, shingoni na kichwani.
Refarii huyo mwenye
umri wa miaka 48 alifariki papo hapo.
Mchezaji mwenza
aliyejaribu kumshawishi asimuue refarii alipa
No comments: