Joh Makin asema hategemei kolabo na wasanii wa nje kutoboa kimataifa.Kolabo nyingine inakuja?
Msanii Joh Makin ni moja kati ya marapa wachache wa Tanzania wanaowika kimataifa hiyo ikichangiwa na kolabo
kadhaa ambazo amezifanya za wasanii wa kimataifa ikiwemo ile ya Don’t Bother aliyofanya na AKA kutoka Afrika kusini.
Hata hivyo rapa huyo kutoka weusi amesema kuwa hategemei kolabo na msanii yeyote yule ili aweze kufika mbali zaidi kwani anaamini hata bila kolabo hizo ndoto yake ingetimia.
“mimi kusema ukweli sikuwahi kujiona sehemu yoyote kupitia kolabo ya mtu,huwa nazichukulia kama ni njia tu Mungu ameweka nipite…kwa mfano hata nisingefanya kolabo yoyote ya kimataifa na mtu yeyote bado isingekwamisha ndoto yangu kwenda pale napotaka kuwa ,naamini ndani yangu Mungu ameweka kila kitu najitosheleza..” alifunguka mweusi huyo na kusema kuwa kuna uwezekano wa kolabo yake na Davido ikasikika si punde.
Source: Ayo Tv
No comments: