Chelsea yapokea kipigigo dhidi ya PSG, lakini wamevunja rekodi hii ya PSG (+Video)
Hatua ya 16 bora ya michuano ya Klabu
Bingwa Ulaya imechezwa usiku wa February 16 kwa michezo miwili kupigwa katika
viwanja vya Parc des Princes na Estádio da Luz, michezo
miwili iliyopigwa usiku huo ni mchezo, kati ya Benfica dhidi ya Zenit St. Petersburg na mchezo wa PSG dhidi ya Chelsea.
Mchezo kati ya Chelsea dhidi ya PSG, ndio ulikuwa
unatajwa kuwa mchezo wenye mvuto zaidi, kwani klabu ya PSG haikuwa na rekodi nzuri katika mechi zao sita,
walizowahi kukutana, Chelsea alikuwa kashinda mara mbili, na
kufungwa mara moja sare ikiwa ni michezo mitatu. Lakini PSG walikuwa na rekodi ya kutokufungwa katika mechi
zake 34 msimu huu ilizocheza katika mashindano.
PSG wamefanikiwa
kubebwa na takwimu yao ya kutofungwa msimu huu, kwani wamefanikiwa kuiadhibu Chelsea kwa jumla ya goli 2-1, magoli ya PSG yalifungwa naZlatan
Ibrahimovic dakika ya 19 na Edinson Cavani dakika ya 78,
wakati Chelseawalifunga goli la kufutia machozi dakika ya 45
kupitia kwa mnigeria John Obi Mikel, goli la Chelsea limevunja
rekodi ya PSG ya kutofungwa goli hata
moja katika michuano yaUEFA msimu huu katika
dimba lake la nyumbani.
Matokeo ya mechi nyingine
·
Benfica 1 – 0 Zenit
St. Petersburg
Video ya magoli ya mechi ya PSG Vs Chelsea
No comments: