Besigye aachiliwa na polisi Uganda
Msemaji wa chama cha
Forum for Democratic Change Ssemujju Ibrahim Nganda amethibitisha kwamba
mgombea urais wa chama hicho Dkt Kizza Besigye aliyekuwa amekamatwa na polisi
sasa ameachiliwa huru.
Kanali huyo mstaafu
ambaye ni kigogo wa upinzani nchini Uganda alikuwa amekamatwa katika kitongoji
cha Naguru, mjini Kampala katika nyumba ambayo upinzani ulidai wizi wa kura
ulikuwa ukifanyika.
Wafuasi wa upinzani,
wakiambatana na kanali Besigye, wanadai walifumania watu wakiiba kura na
wakataka usaidizi wa polisi kukagua nyumba hiyo lakini wakazuiliwa.
Besigye alikamatwa na
maafisa wa polisi walioondoka naye kutoka eneo hilo.
Haijabainika
alipelekwa wapi.
Hii na mara ya pili
kwa Dkt Besigye kukamatwa wiki hii.
Jumatatu, wiki hii
alikamatwa alipokuwa akijaribu
kupitia katika barabara moja mjini Kampala.
Polisi walisema hakuwa na idhini ya kupitia
eneo hilo kwa mujibu wa sheria..
No comments: