Mzungu na watoto wake 19!! bado ana mpango wa kupata wengine

Sue Radford na mume wake Noel wameendelea kukaa kwenye headlines baada ya kutarajia mtoto wa 19 katika familia yao.
Mama huyo raia wa Uingereza mwenye miaka 40 ambaye kwa sasa mtoto wake wa mwisho ana miezi nane, ana ujauzito mwingine wa mtoto wake wa 19.
Hii imekuwa ‘suprise’ kwa watu wanaowazunguka kwa kuwa mwanamke huyo na mumewe mwenye miaka 45 walidai hawataongeza mtoto mwingine baada ya kupata mtoto wao wa 18.
Lakini majirani pamoja na watu wa karibu na familia hiyo wamekuwa hawashangazwi sana na maamuzi ya wazazi hao kwa sababu wenyewe wamekuwa na uwezo wa kuwalea watoto wao kwa kuendesha biashara mbalimbali ambazo zimekuwa zikiwapatia kipato

No comments:

Powered by Blogger.