Sentensi 11 Zilizotolewa Jana na Freeman Mbowe Kwenye Baraza la Idd


Viongozi wakuu wa umoja wa katiba ya wananachi UKAWA wakiongozwa na mwenyekiti wa chama cha Democrasia na maendeleo CHADEMA Mh FREMAN MBOWE pamoja na makamu mwenyekiti wa CHADEMA Profesa SAFARI na kaimu mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF ambaye pia ni mbunge wa bunge la Africa mashariki Mh TWALHA TASLIMA jana jioni walihudhuria Baraza la kuu la idd lililoamndaliwa na Taasisi za kiislam Tanzania, shughuli iliyofanyika katika hotel ya LAMADA Jijini Dar es salaam.
 
Katika shughuli hiyo ambayo iliambatana na dua mbalimbali pamoja na hotuba za viongozi mbalimbali pia walialikwa wagombea urais wa vyama vyote Tanzania lakini hakuna hata mmoja aliyeweza kufika huku mgombea wa UKAWA akiwakilishwa na Mh FREMAN MBOWE.
 
Mh mbowe alipata nafasi ya kutoa Hotuba fupi ambayo iliwagusa mamia ya waislam ambao walikuwa katika shughuli hiyo na hapa nimekunukulia baadhi ya mambo ambayo mbowe aliyazungumza na kushtua wengi

Baadhi ya mambo aliyoongea Mh Freeman Mbowe

1-Nashukuru sana kwa ukaribisho wa shughuli hi,mgombea wetu ndugu EDWARD LOWASA alitamani kuwa nasi jioni hii lakini kutokana na ratiba ya kampeni kubana imebidi aunganishe kwenda kwenye kampeni za kesho huko manyara

2-Swala la mashekh ambao wapo jela bila hukumu yoyote,tulisema siku ya ufunguzi wa kampeni na tunaendelea kusema kuwa tumewaagiza wanasheria wa chama chetu kufwatilia kwa makini na kuona nini hasa kimetokea kwao kama kuna mahali kunahitajika msaada wa kisheria tupo tayari kulishuhulikia hilo kwani sisi lengo letu ni kurudisha umoja na mshikamano Tanzania.

3-Zimebaki siku takribani 30 sasa kabla ya watanzania kufanya maamuzi halisi,ni muda wa maamuzi ndugu watanzania.

4-TANESCO imefilisika na watanzania wengi hawajui hili,sasa shirika la umeme halina hata sent na wameamua kufanya mgao wa kimya kimya lakini ukweli ni kwamba huu mgao ni mkubwa sana huko tuendako kwa sababu hawana hela na wanaficha ukweli,kuna mgao mkali sana sasa wa kimya kimya na utaendelea kuwa mkali kadiri siku zinavyokwenda.

5-Kuna wizi mkubwa sana wa mafuta Tanzania na kuna baadhi ya watu wakubwa wanauratibu wizi huo,Tanzania ina akiba ya mafuta hadi mwezi wa 11 lakini serikali imetoa hati ya kuingiza mafuta nchini ambapo baadhi ya wahusika ni familia ya Rais KIKWETE.

6-Serikali yetu ya awamu ya tano sio serikali ya visasi kama inavyodhaniwa,ila ni serikali ya kuwarudisha watanzania pamoja kwa maridhiano,na maelewano,ila kuna watu itabidi washughulikiwe kwa mijibu wa sheria kutokana na kuligharimu taifa hao tutafanya hivyo.

7-Tume ya uchaguzi ya miezi miwili iliyopita sio tume ya sasa,mwenyekiti yupo ila watendaji wengi wameondolewa bila sababu za msingi.

8-Mtendaji mmoja mkuu wa tume juzi tumepata taarifa kuwa ameondolewa na kupelekwa kusikojulikana na amerudhishwa na kutakiwa kukabidhi ofisi mara moja.

9-Tume ya sasa inaongozwa na wanajeshi na usalama wa taifa,mimi mbowe ndio nasema kama kuna mtu anabisha waje wanikamate leo,hatuwezi kuvumiliana kiasi hiki ni wakati wa kuwekana wazi ili watanzania wafanye jambo wanalolitaka.

10-Nasema hivi hatutakubai hujuma hizi ambazo zinaendelea sasa tutasema hadi mwisho.

11-Mwisho kabisa nasema hivi ni wajibu wetu kutafuta kura,kupiga kura na kulinda kura hivyo ndugu zangu waislam nawaomba tushirikiane katika hili,

ASANTENI KWA KUNISIKILIZA

No comments:

Powered by Blogger.