staili ya lowasa yawashtua wengi

lowasa 1
Mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Ngoyai Lowassa akiwa kwenye daladala.Haruni Sanchawa MGOMBEA urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Ngoyai Lowassa amezua gumzo kubwa baada ya kutumia staili ya kupanda daladala na wananchi wa kawaida, kitu kinachoonekana kuwa ni kampeni ya aina yake
.
Lowassa alifanya zoezi hilo Jumatatu iliyopita ambapo alishuka katika gari lake la kifahari maeneo ya Gongo la Mboto, jijini Dar, akazungumza na waendesha bodaboda na mama lishe wa eneo hilo, kisha kupanda daladala la kwenda Pugu Kajiungeni.
Akiwa ndani ya daladala hilo, Lowassa alizua gumzo la aina yake baada ya abiria kutotarajia kusafiri pamoja na kiongozi huyo ambaye chama chake kinaunda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
“Mh! Hii kali yaani ghafla tu tunashangaa Lowassa huyo ndani ya daladala, hizi siasa za mwaka huu kweli tutashuhudia mengi,” alisema mmoja wa abiria.
Kama hiyo haitoshi, saa chache baada ya Lowassa kufanya tukio hilo la kushtukiza kwa kile kilichoeleza kuwa alikuwa akitaka kujua matatizo ya wananchi, picha za tukio hilo zilizagaa mitandaoni na kusababisha watu waanze kuzijadili.
“Mh! Hii nayo mpya kwani siku zote alikuwa wapi kuyajua matatizo haya? Wanasiasa bwana,” aliandika mdau mmoja mtandaoni.
Lowassa alilifanya ziara hiyo ya ghafla bila hata ya Katibu wa Jimbo la Ukonga, Elkana Pascal na viongozi wengine wa Chadema kuwa na taarifa


No comments:

Powered by Blogger.