mrisho mpoto atafuta nauli kwa kupiga debe kwenye daladala -4
MPENZI msomaji, wiki iliyopita katika simulizi hii ya Mrisho Mpoto tuliishia pale alipotua Dar na mama yake, akaanzishwa Shule ya Msingi, Ilala Boma na kipindi hicho walikuwa maskini wa kutupwa kwani maisha yao yalikuwa ya kwenda
kuokota vifuu, kuni na kuviuza. Songa nayo mwenyewe...
kuokota vifuu, kuni na kuviuza. Songa nayo mwenyewe...
“Mazingira ya nyumba yetu pale Ilala yalikuwa ni kama eneo la kumuelekeza mtu kutokana na jumba bovu nililokuwa nikiishi na mama.”Duh! Lakini ndiyo maisha yalivyo, maisha yakawaje sasa?
“Kipindi chote nikiwa nasoma mama yangu alikuwa akinisihi kitu kimoja, kwamba siruhusiwi kurudi tena Songea kwa namna yoyote ile katika maisha yangu yote na kama nikirudi huko ataniachia ladhi.
“Kipindi chote nikiwa nasoma mama yangu alikuwa akinisihi kitu kimoja, kwamba siruhusiwi kurudi tena Songea kwa namna yoyote ile katika maisha yangu yote na kama nikirudi huko ataniachia ladhi.
“Nikamsikiliza na kuanzia hapo, maisha yangu yakabadilika sana kwani nilipofika darasa la tatu katika shule hiyohiyo ya msingi Ilala Boma, nikaanza kupenda sana kusoma vitabu, kuhadithiwa hadithi pamoja na mashairi. Mbali na hiyo pia nilikuwa nikipenda kujihusisha na kufanya ngonjera na maigizo shuleni.”
Safi sana Mrisho, baada ya hapo? Ina maana kufanya ngonjera na maigizo ndiyo kukakufanya uwe mwanamuziki hadi sasa, namuuliza kichokozi.
Safi sana Mrisho, baada ya hapo? Ina maana kufanya ngonjera na maigizo ndiyo kukakufanya uwe mwanamuziki hadi sasa, namuuliza kichokozi.
“Safari bado ni ndefu sana, nakumbuka katika Runinga ya ITV kulianzishwa kipindi cha sanaa kwa watoto na kipindi hicho, nilikuwa mtoto wa kwanza kukiongoza.“Nikiwa bado katika Kipindi cha Sanaa kwa Watoto, ITV upande wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), wanafunzi chuoni hapo ambao ni Mona Mwakalinga pamoja na Mgunga Mwanyenyelwa walianzisha tamasha kubwa la watoto chuo kikuu lililokuwa likiwakutanisha wanafunzi wengi kutoka shule za msingi mbalimbali kila mwaka.
\“Kupitia tamasha hilo, Mona pamoja na Mwanyenyelwa wakaniona na kugundua kipaji changu.”
Hongera sana kwa hatua hiyo, ikawaje?
Hongera sana kwa hatua hiyo, ikawaje?
“Wakaniambia nina kipaji itabidi niwaoneshe nyumbani kwangu wapafahamu na kuniombea ruhusa kwa mama niwe nao pamoja kila siku mazoezini chuoni hapo. Nikawapeke hadi nyumbani, Ilala. Tulipofika, mama akawakatalia, wakamuomba sana lakini mwisho akaamua kuwakubalia.
“Kwa hiyo nilipofika darasa la nne nilikuwa nikitoka darasani naenda mazoezini kwenye kikundi cha mazoezi hapo chuo ambacho kilikuwa kikihusisha walimu, wanafunzi pamoja na watoto wa pale chuo. Nilikaa kwenye kile kikundi nikifanya mazoezi kwa muda mrefu sana.
“Ikafika mahali mama yangu akawa haoni matunda ya kile kitu nilichokuwa nikikifanya. Nakumbuka kipindi hicho Barabara ya Sam Nujoma (Ubungo-Mwenge) ilikuwa ikitanuliwa na kuwa njia nne na Kampuni ya Konoike ndiyo ilikuwa ikisimamia matengenezo hayo.
“Ikawa rahisi kwangu kwani nilikuwa nikitoka mazoezi na wenzangu tunadandia magari hayo na kwenda hadi Buguruni kisha tunaenda kwa mguu mpaka nyumbani, Ilala.”“Ubungo kuna kituo kilikuwa kinaitwa Minazini (Ofisi za Tanesco), kwa muda mrefu mimi na wenzangu tulikuwa tukipiga debe na kujipatia nauli na hela ya kula. Kuna kipindi ilifikia nakosa nauli ya kwenda mazoezini lakini baadaye, Mona na Mwanyenyelwa wakaninunulia baiskeli ikawa na unafuu wa kutoka Ilala mpaka chuo kikuu kila siku.”
“Mwaka 1994 nikamaliza darasa la saba. Kaka yangu Mashaka yeye baba yake ni mwingine, alikuwa ameoa huko Kigoma, ikabidi nichukuliwe nipelekwe Kigoma nikatafutiwe kazi kwa maana mama yangu aliona ile kazi ya sanaa niliyokuwa nafanya haikuwa kazi na haikuniingizia chochote.”
Je, Mrisho atafika Kigoma? Itakuwaje? Tukutane wiki ijayo kwenye gazeti hilihili
Je, Mrisho atafika Kigoma? Itakuwaje? Tukutane wiki ijayo kwenye gazeti hilihili
No comments: