. Man Utd walipata ushindi wa 3-1 dhidi ya Club Brugge

MAN UTD (1)Mchezaji wa Man Utd, Memphis Depay akishangilia baada ya kusawazisha bao dakika ya 14 kipindi cha kwanza. Man Utd walipata ushindi wa 3-1 dhidi ya Club Brugge ya Ubelgiji katika Uwanja wa Old Trafford usiku wa kuamkima leo
.MAN UTD (4)Marouane Fellaini,  akishangilia baada ya kufunga bao la tatu dakika ya 90 kipindi cha pili.MAN UTD (5)
Mashabiki wa Club Brugge ya Ubelgiji wakishangilia baada ya kupata bao lao la kwanza dakika ya nane kipindi cha kwanza.MAN UTD (6)Kocha wa zamani wa Man Utd, Sir Alex Ferguson (katikati).MAN UTD (7)Wachezaji wa Man Utd wakishangilia kwa pamoja.Manchester United imeanza vizuri mchezo wa kwanza wa mchujo kuwania nafasi kuingia hatua ya makundi ya michunao ya klabu bingwa barani ulaya,Baada ya kupata ushindi wa 3-1 dhidi ya Club Brugge ya Ubelgiji. Brugge ilipata bao lao mapema dakika ya 8 ya mchezo baada ya kiungo wa Man Utd, Michael Carrick kujifunga.Mshambuliaji mpya wa kikosi hicho cha mashetani wekundu Memphis Depay akasawazisha bao hilo dakika ya 14 kabla ya kuongeza bao la pili dakika 43, kiungo aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Wayne Rooney, MbelgijiMarouane Fellaini, akifunga bao la tatu lilihitimisha ushindi huo.Matokeo mengine ya michezo ya mchujo kuwania kuingia hatua ya makundi ya klabu bingwa ulaya ni:Astana 1 APOEL Nicosia 0BATE Borisov 1 Partizan Belgrade 0Lazio 1 Bayer Leverkusen 0Sporting CP 2 CSKA Moscow 1

No comments:

Powered by Blogger.