Wakala_Wa_Shetani-3-

KWA TAARIFA
ZAIDI NICHEKI HAPA 0785848566
Ndipo siku ya kujifungua
ilipowadia hakutaka aitwe mtu yeyote kushuhudia anazaliwa mtoto gani kwa
kuhofia siri yake kutoka nje kama atajifungua mtoto albino. Mumewe baada ya
kukatazwa na mkewe asimwite mtu yeyoye aliamua kumsaidia mkewe kujifungua. SASA
ENDELEA...
SHARE NIPOST MWENDELEZO WAKE
ONYESHA UPENDO KIPANDE KITAKACHOENDELEA
Kwa vile alikuwa na uzoefu
aliweza kumsaidia mkewe kujifungua mtoto salama. Baada ya huduma zote mtoto
alilazwa pembeni huku wakijitahidi kuzuia sauti ya mtoto kabla ya kujua mtoto
aliyezaliwa ni wa aina gani ni albino au wa kawaida.
Mathayo baada ya kumhudumia mtoto
wake na mkewe ambaye aliweza kukaa mwenyewe, kazi akawa kumtazama mtoto
aliyezaliwa wa aina gani. Uchunguzi ulionesha mtoto yule ni albino. Walijikuta
wote wakikosa raha hasa ngw’ana Bupilipili ambaye aliamini ana mtihani mkubwa
wa kumpoteza tena mtoto mwingine ambaye amekaa naye tumboni kwa kipindi kirefu
halafu watu wamchukue na kwenda kumuua kiurahisi.
“Unaona sasa mume wangu,
ungemwita mama Sabina lazima siri hii ingetoka nje.”
“Sasa tutafanyaje na hali hii imetokea?”
“Dawa ni kumficha mtoto wetu ili wasijue nimejifungua.”
“Tutamfichaje? Pia mtu aliyejifungua anajulikana kwa tumbo kupungua na mtoto wetu tutamlea vipi usionekane kwa watu?” Mathayo aliona mtihani mgumu.

“Mume wangu nitaendelea kuweka
nguo tumboni siku zote ili lionekane kubwa.”
“Tumbo sawa litaonekana kubwa, mtoto tutamweka wapi? Tukimficha ndani lazima atalia na kutoa sauti majirani watataka kujua ni mtoto wa aina gani. Na wakimuona hawatakubali kumuacha lazima watamuua, pia kutupiga faini ya ng’ombe watano huoni kama zizini kwetu ng’ombe watapungua?”

“Hilo nililijua toka mwanzo na
nilijipanga kwa ajili ya hili,” ngw’ana Bupilipili alimtoa hofu mumewe aliyeonekana
kuchanganyikiwa zaidi.
“Tutafanyaje mke wangu, huwezi kuamini hapa akili haifanyi kazi kabisa, siwezi kupoteza mtoto wa pili hivi hivi. Mke wangu sikubali nitaua mtu safari hii siwezi kukubali mtoto wangu auawe,” Mathayo alisema kwa uchungu kumuunga mkono mkewe.

“Nimepanga kitu kimoja kama
nitajifungua albino.”
“Kipi hicho?” Mathayo aliuliza kwa shauku ya kujua mke wake amepanga nini.
“Usiku huu tutakwenda hadi kwenye mlima wa karibu na shamba letu, kuna pango nimeliandaa kwa ajili ya kumficha mtoto wetu.”
“Kipi hicho?” Mathayo aliuliza kwa shauku ya kujua mke wake amepanga nini.
“Usiku huu tutakwenda hadi kwenye mlima wa karibu na shamba letu, kuna pango nimeliandaa kwa ajili ya kumficha mtoto wetu.”
“Mke wangu unataka kuniambia
usiku huu tutamwacha mtoto peke yake kisha turudi nyumbani?”
“Hapana, kila siku tutatoka alfajiri hadi kwenye pango hilo, kisha wewe utaingia shambani nami nitakuwa karibu na mtoto mpaka atakapokua kidogo, tutatoroka usiku kwa usiku na kwenda kijiji kingine.”
“Hapana, kila siku tutatoka alfajiri hadi kwenye pango hilo, kisha wewe utaingia shambani nami nitakuwa karibu na mtoto mpaka atakapokua kidogo, tutatoroka usiku kwa usiku na kwenda kijiji kingine.”
“Lakini mke wangu ni kijiji gani
tutakachoweza kuishi na mtoto huyu bila matatizo?”
“Mume wangu hebu tufanya hili kwanza mengine yatafuata baadaye.”
“Mume wangu hebu tufanya hili kwanza mengine yatafuata baadaye.”
Usiku uleule walimchukua mtoto
wao na kutoka naye kiza kwa kiza. Japokuwa usiku ulikuwa mkubwa wenye kutisha,
Ngw’ana Bupilipili alionesha ujasiri wa ajabu kwa kumuongoza mumewe hadi
shambani kwao ambapo pembeni yake kulikuwa na kilima kidogo ambacho ndipo
alipoandaa pango la kumtunzia mtoto wao.
Walitumia majani makavu kuyawasha
moto ili kutengeneza tochi ya dharula kumulika sehemu ile. Mumewe alishangaa
kukuta sehemu ile imetengenezwa vizuri sana.
“Mke wangu umetengeneza lini
huku?”
“Toka nilipopata wazo la kujifungua tena mtoto albino basi nilijawa na mawazo ya kunusuru maisha ya mwanangu na kupata wazo la kupatengeneza huku.”
“Toka nilipopata wazo la kujifungua tena mtoto albino basi nilijawa na mawazo ya kunusuru maisha ya mwanangu na kupata wazo la kupatengeneza huku.”
Walimlaza vizuri mtoto wao kisha
Ngw’ana Bupilipili alijilaza pembeni ya mwanaye, naye Mathayo alilala pembeni
kidogo ya mkewe, kwa vile muda ulikuwa bado usingizi uliwapitia.
Waliamshwa na sauti ya mtoto
aliyekuwa akilia, Ngw’ana Bupilipili alishtuka usingizini na kukuta kumeanza
kupambazuka, alimnyonyesha mtoto wake aliyeonekana ana njaa. Wakati huo mume
wake alikuwa amekwisha amka na kutoka nje kuangalia hali ya usalama.
“Mke wangu wacha nirudi nyumbani
nikawaandalieni chochote kitu.”
“Hakuna tatizo usisahau dawa zangu tumbo nalisikia kwa mbali.”
“Hakuna tatizo mke wangu.”
“Hakuna tatizo usisahau dawa zangu tumbo nalisikia kwa mbali.”
“Hakuna tatizo mke wangu.”
Mathayo kabla ya kuondoka
alimtazama mkewe na kisha mtoto wake ambaye hakuwa na habari yeyote zaidi ya
kuchezesha mikono na miguu baada ya kushiba na kufurahi kuja dunia salama, bila
kujua hatari iliyo mbele yake ya kuonekana mkosi kwa jamii.
Bila kutegemea machozi yalimtoka kumwonea huruma mkewe ambaye aliamua kuishi maisha ya siyo yake kuhofia uhai wa mtoto wao.
Bila kutegemea machozi yalimtoka kumwonea huruma mkewe ambaye aliamua kuishi maisha ya siyo yake kuhofia uhai wa mtoto wao.
Pia alimuonea huruma mtoto wao
ambaye bado alikuwa hajapewa jina kutokana na misukosuko ya moyo wa kutaka
kuokoa kwanza maisha yake baada ya wanakijiji kuona watoto maalbino ni mkosi
kama wakiachwa kijiji kitapata balaa kubwa.
Japokuwa awali naye alikuwa ni
mmoja wa watu walioamini albino ni mkosi, lakini mambo yalibadilika baada ya
kutokewa yeye. Mwanzo naye alishiriki kuwaua watoto wa wenzake. Siku zote msiba
wa mwenzio hauumi lakini msiba ikiwa kwako utajua uchungu wake. Mathayo baada
ya mkewe kujifungua mtoto wa kwanza albino alikubali auawe lakini mkewe
alisimama kidete asiuawe na kuwa tayari wafukuzwe kijijini.
Wakati wanahama kijiji
walipovamiwa na vijana wa kijiji wenye jukumu kusaka na kutoa uchafu wa watoto
wanaoonekana wanaleta mikosi kijijini. Mtoto albino alipouawa nyumba ilifanyiwa
tambiko na kutengwa kwa muda wa wiki mbili.
Kilio cha mkewe baada ya kubeba
ujauzito wa pili cha kuhofia uhai wa mtoto wake kilimfanya Mathayo naye abadili
uamuzi na kuwa tayari kukisaliti kijiji pindi mkewe atakapo kifungua mtoto
albino. Aliapa moyoni hatakubali kumtoa mtoto wake auawe tena.
Michirizi ya machozi iliendelea
kumtoka huku miguu ikiwa mizito kunyanyuka. Mkewe alimwona na kunyanyuka
alipokuwa amejilaza na mtoto na kumfuata mumewe. Alimkumbatia na kumbembeleza
huku akimpigapiga mgongoni taratibu.
“Mume wangu hii ni mitihani
aliyotupa Mungu tunatakiwa kupambana nayo, tunatakiwa tumtegemee yeye kwa kila
kitu na kumtumai kwenye majaribu mazito kama haya. Hakika tutashinda japo kukua
mwenetu itakuwa sawa kabisa na ngamia kupita kwenye tundu la shindano. Lakini
tukimuamini yeye lolote kwake linawezekana,” Ngw’ana Bupilipili alimpa moyo
mumewe.
“Ni kweli la..la..kini...” Mathayo hakumalizia kutokana na donge la uchungu kumkaba kooni huku machozi yakimdondokea mkewe.
“Ni kweli la..la..kini...” Mathayo hakumalizia kutokana na donge la uchungu kumkaba kooni huku machozi yakimdondokea mkewe.
Etaendelea
No comments: