Wakala_Wa_Shetani -1-
KWA TAARIFA ZAIDI NICHEKI HAPA 0785848566
UTANGULIZI:
KILA binadamu yupo duniani kwa ajili ya kuishi. Hakuna aliyeumbwa kupata mali kwa ajili ya kumpoteza mwenzake bali imeumbwa riziki ya mtu ipitie kwa mtu. Wengi wamesahau kila kiumbe kitaonja mauti siku yake ikifika lakini si kwa utashi au tamaa za watu bali kwa mapenzi ya Mungu. Wengi huamini wataishi milele na kuwageuza wenzao kama chambo au ngazi ya kufikia utajiri au mafanikio kwa vile uhai wao unanukia harufu ya fedha. Ili kujua kwa nini uhai wa watu wengine una harufu ya fedha ungana tena na yuleyule mwandishi wako mahiri katika riwaya nyingine ya kusisimua…
TUWE PAMOJA…

Kilikuwa kiumbe cha ajabu ambacho japokuwa kilifanana na umbile
la kibinadamu lakini kilikuwa na matendo ya kinyama. Wengi walifikiri ni mzimu
lakini haukuwa mzimu, alikuwa binadamu tena albino ambaye alionekana kuishi
maisha marefu kama mnyama wa porini huku akiwa hana kiungo kimoja cha mwili,
mkono wa kulia.
Umbile lake lilikuwa lenye afya njema, akiwa na nywele nyingi
nyeupe na ndefu kama rasta. Ndevu nyingi, kucha ndefu na mavazi yaliyochakaa
yaliyoonesha kutojua maji kwa kipindi kirefu zaidi ya mvua iliyomnyeshea.
Chakula chake kilikuwa nyama mbichi na matunda ya msituni. Macho
yake yaliyokuwa mekundu na muda mwingi aliangalia chini. Alionekana kuwachukia
binadamu kuliko kitu chochote.
Siku ya kwanza kukutana naye, aliua watu zaidi ya watatu, ikabidi itumike nguvu kwa kumpiga risasi ya kupoteza fahamu ndipo walipoweza kumkamata.
Siku ya kwanza kukutana naye, aliua watu zaidi ya watatu, ikabidi itumike nguvu kwa kumpiga risasi ya kupoteza fahamu ndipo walipoweza kumkamata.
Daktari aliyepelekwa kwa ajili ya kumchunguza alinyongwa kwa
kamba alizokuwa amefungwa nazo. Japo alikuwa kiumbe wa kawaida lakini mazingira
yalimfanya aonekane kama mnyama. Baada ya kumkata nywele na kucha, bado
alionekana mtu mwenye hasira, asiyependa kutazama watu usoni.
Mkono mmoja uliokuwa umekatwa ulibaki na kovu la muda mrefu,
lingekuwa bichi labda wangesema ni mmoja wa majeruhi wa kukatwa kiungo cha
mkono katika janga lililolikumba taifa la kuuawa kwa kukatwa viungo walemavu wa
ngozi, albino.
Lakini alionekana mtu aliyeishi maisha ya porini kwa kipindi kirefu japo haikufahamika ni muda gani alioishi porini.
Lakini alionekana mtu aliyeishi maisha ya porini kwa kipindi kirefu japo haikufahamika ni muda gani alioishi porini.
Kingine kilichowashangaza watu ni hali ya kuwa kama mnyama
asiyependa wanadamu zaidi ya wanyama. Tofauti yake nyingine, alikuwa na roho
mbaya kuliko ya simba.
Hakupenda chakula kilichopikwa, alipenda vyakula vibichi kama nyama mbichi na matunda, hivyo ndivyo vilikuwa vyakula vyake vikuu.
Hakupenda chakula kilichopikwa, alipenda vyakula vibichi kama nyama mbichi na matunda, hivyo ndivyo vilikuwa vyakula vyake vikuu.
Wataalamu wa kujua matatizo ya binadamu walikutana na
kumchunguza kwa muda. Vipimo vyote vilionesha yupo katika hali ya kawaida. Umri
wake ulionesha kuwa na miaka kati ya 35 na 40. Mmoja wa wataalamu aligundua
kuwa mtu yule aliishi maisha ya porini kwa muda mrefu hali iliyosababisha awe
na hulka kama mnyama.
Walikubaliana kumtengenezea mazingira ya kumrudisha katika hali
ya ubinadamu. Pamoja na kuwa haongei lakini alionesha dalili za kusikia kwani
alikuwa makini kusikiliza kila kilichokuwa kikizungumzwa.
Mtaalamu wa saikolojia ya binadamu aliwaeleza kuwa baada ya muda atarudi katika hali ya kawaida na kuamini mtu yule alikuwa na siri nzito ya kumfanya aishi maisha kama mnyama kwa muda mrefu porini na kuwa kiumbe mwenye hasira, asiyependa kutazama watu machoni.

Walimtengenezea mazingira ya upendo huku muda wote akiachwa peke
yake akiwa amewekewa muziki wa taratibu wa vyombo vitupu. Mtaalamu aliwaambia
kupitia muziki wa vyombo vitupu, taratibu ataanza kujengeka kifikra na kujiona
ni binadamu. Pia walikuwa wakimwekea picha za sinema zenye kuonesha maisha ya
upendo ya watu tofauti wakiwemo albino na watu wa kawaida.
***
Mtu yule aligunduliwa katika msitu mnene pembezoni mwa Mji wa Mangu na wataalamu wa masuala ya utengenezaji wa mvua ambao waliletwa nchini kukabiliana na ukame baada ya taifa kukumbwa na janga kubwa la ukame uliosababisha mabwawa ya maji katika vyanzo vya umeme kukauka, hali iliyosababisha mgao mkubwa wa umeme.

Marafiki wahisani wa nchi zilizoendelea, walijitolea kuleta
wataalamu wake kwa ajili ya kutengeneza mvua kwa bei nafuu. Nchi ya Thailand,
moja ya marafiki walikubali kusaidia wataalamu pamoja na mitambo ili kumaliza
tatizo la ukame lililoikumba nchi yetu iliyokuwa katika hatari ya kuingia
gizani baada ya mabwawa yote kuwa
kwenye hali mbaya kwa kina cha maji kuendelea kupungua kila
kukicha.
Kikosi cha wataalamu kilizunguka sehemu yenye milima yenye miti mingi ambayo wangeweza kuitumia kutengeneza mvua. Msitu wa Nyashana uliokuwa pembezoni mwa Mji wa Mangu ulionekana kufaa kuzalishia mvua.
Baada ya kuuchagua msitu ule, kazi ilianza mara moja kwa kuanza kupima. Wakiwa wanapima kwa kutumia kiona mbali, waliweza kumuona mtu ambaye baada ya kumvuta karibu kwa mitambo ya kiona mbali, walihisi ni mzimu, wakashawishika kusogea karibu zaidi ili wamuone vizuri.

Walipomkaribia yule mtu ambaye wao walijua ni mzimu, alikimbia
na kupotelea mapangoni. Walisitisha kazi ya kupima na kuanza kumtafuta yule mtu
kutaka kujua mwisho wake na kwa nini yupo sehemu ile. Siku ya kwanza, mpaka
giza linaingia hawakufanikiwa kumuona.
Wataalamu hawakukubali kumkosa, wakapanga kurudi siku ya pili alfajiri na kujificha. Walifanikiwa kumuona majira ya saa moja asubuhi akitoka kwenye pango lake, akawa anajinyoosha mwili.
Wataalamu hawakukubali kumkosa, wakapanga kurudi siku ya pili alfajiri na kujificha. Walifanikiwa kumuona majira ya saa moja asubuhi akitoka kwenye pango lake, akawa anajinyoosha mwili.
Alipopiga miayo, meno yake yalionekana yamebadilika rangi na
kuwa kama ya simba. Weupe wa meno yake ulipotea kabisa. Mzungu mmoja
alijitokeza mbele yake, yule mtu alipomuona alishtuka na kutimua mbio kwa
kukwea miti na mawe kwa mkono mmoja kama sokwe.
Kila mmoja alipigwa na butwaa na kujiuliza kwa nini mtu yule yuko vile, suala ya mzimu walilifuta japo alikuwa na nywele nyingi ndefu, kucha ndefu na nguo chakavu.
Kila mmoja alipigwa na butwaa na kujiuliza kwa nini mtu yule yuko vile, suala ya mzimu walilifuta japo alikuwa na nywele nyingi ndefu, kucha ndefu na nguo chakavu.
Wapo waliodhani ni msukule, baada ya kukimbia waliingia sehemu
aliyotoka, ndani ya pango lililokuwa na giza nene. Kwa msaada wa tochi yenye
mwanga mkali, walifika hadi ndani ya pango. Ndani ya pango hilo walikuta mifupa
mingi ya wanyama, matunda yaliyoliwa nusu na nguo chakavu zilizokuwa kama
godoro.
Hawakuishia hapo, walizunguka kila kona lakini hawakukuta kitu kingine zaidi ya vile vitu walivyoviona. Kutokana na kuonekana mtu yule ni vigumu kumkamata, walitengeneza mtego na kuondoka.
Hawakuishia hapo, walizunguka kila kona lakini hawakukuta kitu kingine zaidi ya vile vitu walivyoviona. Kutokana na kuonekana mtu yule ni vigumu kumkamata, walitengeneza mtego na kuondoka.
Itaendelea.......

No comments: