MTOTO WA HAYATI - Sehemu Ya 2



 Mtunzi..... MoonBoy

Simu No. +255714419487 WhatsApp

Ilipoishia Jana →↓↓

Nilizidi kua na hofu huku nikinyata nyata ili niweze kuwasogelea karibu, lakini wazo langu lililopo kichwani ni kwamba, mimi najua ni baba na mama watakua wanacheza bao na jirani, hivyo nilikua nawamendea ili niwashtue, maana mama na baba wana tabia ya kucheza bao usiku, japo sio usiku mkubwa kama leo hiii, niliendelea kuinama huku nikijificha kwenye gadeni na maua yaliopo hapo, nilikua nahisi baridi sana, kwani nilitoka na boxer tu,......  Lakini nilipofika karibu nilishindwa kuelewa hawa wazazi wangu wanacheza bao gani, mbona sioni hata wakirusha rusha mikono zaidi ya kuona mikono ikiwa juu juu tu.......  Nilijipa moyo kua huenda ni mchezo mpya waliougundua watu hawa, maana si wazee wa zamani hivyo watakua wakijua michezo mingi mno,.....  Nilizidi kusogea mpaka nikakaribia karibu yao huku nikiwa nimejificha kwenye shina la ua moja kubwaaaa, lakini baridi ndio ilikua inanisumbua hivyo nikawa natetemeka sana huku,  nikiwa nataka niwashtue baba na mama kama vile tunacheza kombolela,

ENDELEA...........


Nilikua sio mkubwa kama unavyofikiri, kana kwamba labda michezo ya kitoto nimeacha lahasha, bali nilikua ni mtoto mwenye umri wa miaka 14 tena umbo langu lilivyokua dogo unaweza kusema nina miaka 10 au 11, yaani nilikua nipo kidato cha kwanza lakini akili ya kiutu uzima ilikua bado haijanijia, hivyo ukiniangalia tu utanichukulia kama mtoto kabisa, japo miaka kumi na nne kwa msicha ni mdada mkubwa tu, na hata mimba anapokea vizuri tu, ila kwa wakiume mwenye unri wa miaka 14 hawezi kutungisha mimba, kataa kubali lakini ukweli ndio huo,

Sasa nilipokua nazidi kusogea maeneo yale, nilishangaa kuona mtu katikati tena walikua wskimwagia unga, huku wakimpiga vibao vya kichwa, tena cha ajabu zaidi ni kwamba wale watu watatu ambao wamemzunguka huyo mtu ambae sikumjua kwa sura, walikua wapo uchi wa mnyama, sasa nikajiuliza kua, huu ni mchezo gani ambao wameugundua watu hawa, tena mchezo wa usiku mida ya saa nane,....  Sasa nikiwa naendelea kuangalia, ghafla niliona kisu kilichojikunja ambacho kilishikwa na mama mmoja ambae nilikua namuona kwa nyuma, maana nilikua nyuma ya mgongo wa huyo mama, Nilishangaa kila kisu kikinyanyuliwa na kumpata yule mtu aliekua pale chini tena, sasa kilivyompata yule mtu aliguna, na kugundua kua alikua ni wa kiume,...  Sasa nilipoona anarudia tena kumpiga na kile kisu, mimi niliamka na kuanza kukimbia kana kwamba niliogopa sana kwa kuuona ukatili ule uliokua ukifanyika maeneo hayo,
Sasa kile kitendo cha kukurupuka na kukimbia kiliwashitua wale watu, ila sikua nimeangalia nyuma kwa haraka ila nilipofika karibu na mlango niligeuka huku niliwa naingia ndani, lakini cha ajabu sikuweza kuona mtu maeneo yale, yaani sijui walipotea poteaje maeneo yale, sasa hicho ndicho kilichonifanya nizidi kua muoga zaidi kuliko mwanzo, nilifunga mlango na kuingia chumbani kwangu kisha nikalivuta shuka kwa uoga huku nikitetemeka kwa uoga,  Nilijifunika brangeti huku nikiwa nimejikunja utafikiri mtu anaesikia baridi, Hata usingizi haukua ukija kwa urahisi,

Kesho yake asubuhi nilikua nipo zangu chumbani nikijiandaa kwenda shule, Tulikua tuna housegirl ambae alikua akinisambazia chai ili ninywe niende shule, Mtoto wa kiume nilipiga chai mida hio huku nikiwaza kupewa pesa ya kula sambusa shuleni,...  Nilipomaliza nilichukua begi langu kisha nikaliweka begani kisha huyoo nikawa natoka zangu,
Sasa nilipokua natoka mlango mkubwa, ili niende nikasubirie school bus, niliskia sauti ikitokea chumbani kwetu huku ikiita
"dada, dada"
Ilikua ni sauti ya mama angu ikimuita mamkubwa ambae alikua ni mgeni tena mgeni wa jana tu,
"abeeeee"
"jamani baba sheby sjui ana nini kazidiwa"
Niliposikia tu hivyo nami sikutaka kuendelea kwenda shule bali niligeuza na kwenda chumbani kwa akina baba,

Kwwli nilimkuta baba yupo hoi, tena alikua hata kuongea hawezi....  Chapuchapu mama alienda kuwasha gari uwani na kuliweka sawa kisha tukamuingiza ndani ya gari, nami sikua nyuma kabisa, nililiacha begi langu nyumbani kisha nami nikaingia kwenye gari, safari kuelekea hospitalini japo mama alinikataza lakini niligoma kukaa nyumbani,............  Nyumbani aliachwa housegirl tu, na kwenye gari tulikua mimi mamkubwa na mama angu, mama alikua akilia sana huku mamkubwa nae akiwa analia kwa uchungu,.......  Tulifika hospitalini kisha manesi walileta machela na kumuingiza wodini, sisi watu watatu tulibaki nje tukisubiria taarifa sahihi kuhusiana na huko ndani kunaendeleaje,

Tulikaa nje zaidi ya masaa mawili, huku madokta wakipita pita na madripu ya damu na maji kwa ajili ya kumuudumia baba anfu, mama alikua hakai kila akimuona dokta, tuliendelea kukaa hapo hospitalini bila majibu yeyote yale ambayo yangeturidhisha kwa namna moja ama nyingine,. Na muda huo nilikua nipo na yunifom za shule,

Ilipofika saa tano na nusu asubuhi, ndio dokta anatoka huku akiwa anavua gropsi zake, mimi na mama angu tulikurupuka na kumfata dokta,
"dokta vp, mume wangu anaendeleaje?"
"aaaaa Anaendelea vizuri na mnaweza kwenda kumuona"
Lakini baada ya dokta kusema hivyo, nilimsikia mamkubwa akiuliza huku akitoa macho
"unasemaje dokta? Mungu wangu afadhali shemeji yangu apone"
Sikua nikiwaza chochote kile bali mimi ndio nilikua na spidi ya kuingia katika hio wodi ambayo ndio alilazwa baba yangu,
"baba, unanini baba angu"
"mwanangu sheby, hata mimi mwenyewe sijui, kwani vilinijia gafla tu bin vuu"
Mara mama nae alifika na kumkumbatia baba pale pale kitandani, huku akimuuliza juu ya hali yake hio aliokua nayo, Pia mamkubwa alikua akiongea nae kwa uchungu sana huku huku akimshika shika, lakini mimi sikua na wazo lolote lile linaloendelea,

Sasa nikiwa nimekaa pembeni ya baba hapo hapo kitandani, niliikumbuka ile ndoto ya jana, sasa nikawa najiuliza kua
"ivi ile ilikua ni ndoto au kweli"
Sasa niliposema hivyo mamkubwa alidakia juu kwa juu huku akisema kua
"hio itakua ni ndoto mwanangu"
"heeeee kwani wewe unaijua hio ndoto"
Nilimuuliza hilo swali huku nikimuona akijibalaguza balaguza na kucheka cheka,
"unajua wewe ni mtoto wangu, hivyo ukiota tu lazima namimi nijue maana damu ni moja na wewe"
Aliongea hivyo huku akicheka cheka kinafiki, na mama pia alikua akimsapoti, wakati huo baba alikua akinywa chai ya maziwa kwa sambusa na chapati za mayai,
"lakini hapana, kama ni ndoto tu nisingechubuka goti"
Sasa kile kitendo cha kusema kua nisingechubuka goti kilimshtua sana mama angu na kumfanya aniulize huku akinipandisha suruali amvayo nilikua nimevaa ili aone hilo jeraha ambalo niliumia wakati wa ndoto,
"sheby, umeumia wapi baba"
"nimeumia kwenye goti hili la kulia"
"jamaaani we mtoto umefanyaje, hebu twende kwa dokta mara moja"
Mama alinivuta pale nilipokua nimekaa huku akitaka kutoka kwenda kuniripoti kwa dokta ili nipate matibabu, na huo ulikua ni mchubuko kidogo tu yaani haupaswi hata kwenda hospitali wala kupewa dawa, lakini kwa jinsi wazazi wangu walivyokua wakinipenda, waliona mchubuko ule ulikua ni bonge la kidonda kwa upande wao,

Sasa nilipokua natoka nilimuona mamkubwa akiniangalia kwa jicho baya kana kwamba kama vile kuna kitu ananionya,....  Huezi amini nilijikuta nasita kwenda kumuona dokta, afu hapo hapo nikakumbuka kua katika ule mkono uliokua umenyanyua kile kitu usiku ule ulikua una bangili flani aina ya waya kopa yaani bangili iliokunjwa ila haikua ya kununua dukani kama tulivyozea kuona wadada zetu wakizivaa, na bangili hizo hua zinapendwa sana kuvaliwa na watu wenye asili ya uganga, kwani niliwahi kuziona siku moja tulipoendaga tanga kusalimia, mmoja wa ndugu zetu alikua ni mganga, na ndipo nilipoanza kuziona, sasa leo ndio nimeiona moja katika mkono wa kushoto wa mamkubwa na bangili hio niliiona hata jana usiku katika wale watu watatu waliokua wamemzingira yule mtu,.... .

Sasa baada ya kuona ile bangili pamoja na vile alivyonikazia macho nilisita kwenda huko kwa dokta, maana tulikua tunamuacha baba na mamkubwa wenyewe, hivyo kuna akili ikanijia ghafla ya kutokwenda....
"sheby, twende dokta akapaone jamani"
"mamaa hapo hapana shida turudi tu"
Mara mamkubwa akadakia juu kwa juu
"mwanangu sheby, we nenda ukapewe dawa mwanangu"
Sasa nikiwa navutana na mama, nilimponyoka na kukimbilia kwa baba kisha nikaanza kumkagua kichwa kama ana alama ya yeyote ile kichwani, lakini hakua na alama yeyote ile,
"we sheby unanikagua nini"
Baba aliniuliza hivyo huku akijishika kichwa chake na yeye akijikagua,

Sasa kile kitendo kilimchukiza sana mamkubwa, kwani nilimuona akikasirika ghafla na kuniangalia kwa jicho baya, ilibaki kidogo tu nimuulize kua kwanini ananiangalia sana,
Mama angu alinirudia tena na kunishika mkono kwenda kwa dokta, Mara na mamkubwa nae akaamka,  sasa tukawa tunaenda wote kwa dokta, kwani roho yangu iliridhika baada ya kumuona nae katoka pale wodini, maana roho yangu ilikua haitaki kabisa kumuacha mamkubwa na baba pale wodini na sijui ni kwanini

Tulipofika kwa dokta mama alitoa maelezo kuusu mimi goti langu lilivyochubuka,
"mmmhh mama kweli unamjali mwanao, yaani mchubuko huu unataka apewe dawa?"
"dokta, kidonda ni kidonda hata kama ni kidogo"
Mara mamkubwa nae akasapoti kua
"ni kweli, maana kinaweza kua kikubwa baadae"
Basi dokta akaanza kunitaftia dawa huku wakiongea mengi kuusu mimi, dokta aliniuliza kua nimechubuka na nini, nikamwambia nilikua nacheza mpira ndio nikachubuka, lakini haikua kweli, bali nilichubuka jana usiku pale nilipokurupuka na kukimbia baada ya lile tukio la usiku ambalo mpaka sasa bado sijalipatia jibu kua ilikua ni ndoto au ni kweli, na kama ni ndoto mbona nimechubuka goti, au nimejigonga ukutani nilipokua naota, nilijiuliza maswali mengi sana juu ya swala kama hilo,

Sasa nikiwa naendelea kupewa matibabu ya goti, mara mamkubwa alimuuliza dokta  kua
"dokta, choo chenu kipo wapi"
"aaaa choo kipo kulia ukishapita hio kordo hapo mbele yake kuna vyoo"
"ok asante"
Nilimwambia mama kua tuondoke zetu
"mama, twende kwa baba"
"hebu subiri utibiwe we mtoto"
"mama mi staki matibabu tena"
Mara dokta akadakia juu kwa juu
"dogo tulia namalizia kukufunga bendeji tu"
Yaani kile kitendo cha mamkubwa kuondoka roho yangu ilikua ikidunda mno,
"sheby kwani una nini lakini"
"mamkubwa anaenda wapi"
"si anaenda msalani, kwani hujasikia hapo akiulizia uwani"
"mamaaa we twende bwana"
"nitakuchapa sasa pumbavu wewe, kikiwa kikubwa hiki utamsumbua nani? Hebu tulia mwehu wewe"
Nilitulia lakini sikua na amani kabisa juu ya mamkubwa kuenda uwani,


Itaendelea

No comments:

Powered by Blogger.