UTAPENDA ALICHOKIONGEA RAIS MAGUFULI KWENYE KIKAO CHA HALMASHAURI KUU YA TAIFA 'NEC' KWELI HUYU RAIS MAGUFULI ANABALAA ZITO


Kikao cha halmashauri kuu ya Taifa ‘NEC’ ya chama cha mapinduzi ‘CCM’ kimekutana leo December 13 2016 ikulu jijini Dar es salaam ikiwa ni kikao cha kwanza kuongozwa na Rais Magufuli tangu achaguliwe kukiongoza chama hicho tawala July mwaka huu. Hizi ni baadhi tu ya kauli alizozitoa mwenyekiti wa chama hicho Rais Magufuli
'Sioni aibu ya kuwakaribisha wanaCCM hapa Ikulu maana bila ninyi nisingefika hapa, hapa ni mahali pa watanzania wote'-JPM 
'Vyama vingine wakitaka kufanya vikao hapa Ikulu waombe ila tutataka kujua ajenda zao'-JPM 
'Hii haitakuwa mara ya mwisho tutakapoamua hakuna mtu atakayenipangia nifanyie mkutano wapi'-JPM 
'Hatutaki kuwa na chama legelege cha watu walalamikaji, sisi ndio tumepewa ridhaa na wananchi kuongoza'-JPM 
'Nitapenda chama changu CCM kizingatie kanuni za uchaguzi ikwemo kanuni ya kiongozi kuwa na nafasi moja tu ya uongozi-JPM 
'Nitapenda kuwa na jumuiya za chama zinazozingatia matakwa ya chama'- JPM 
'Napenda tuwe na chama kinachoongozwa na wanachama na sio chama kuongozwa na mtu chama ni mali ya wanachama'- JPM 
'Tunataka kununua meli mbili, moja ziwa Tanganyika na nyingine ziwa Victoria' -JPM 
'Tunataka chama chetu kijitegemee kiuchumi, ni aibu kutegemea fedha za ruzuku na watu binafsi ili kujiendesha' -JPM 
'Rasimali nyingi hatunufaiki nazo kutokana na mikataba isiyo na tija, usimamizi mbovu na ubadhirifu'-JPM 
'Wapo wananchama wachache ambao ukisaliti chama chetu hasa kipindi cha uchaguzi na wengine kuendeleza makundi'-JPM 
'Napongeza kamati za siasa za wilaya, mikoa ambazo zimechukua hatua dhidi ya waliotusaliti kwenye uchaguzi mwaka jana-JPM 
'Katika awamu hii hatutamsamehe mtu yeyote wa kutafuta uongozi kwa njia ya rushwa' JPM 
'Nina uhakika zaidi ya viwanja sita katika nchi hii tutaviwekea lami, tumeanza na Dodoma'-JPM 
'Bei ya korosho imepanda kutoka 1000 hadi 4000 kwa kg 1 na walivyo wale watani zangu wameamua kuwanywesha mbuzi bia-JPM 
'Bei ya korosho imepanda kutoka 1000 hadi 4000 kwa kg 1 na walivyo wale watani zangu wameamua kuwanywesha mbuzi bia-JPM 
'Nimeshapata mialiko karibu ya 50 lakini nimeamua kusafisha nyumba yangu kwanza kabla ya kwenda kusafisha kwa jirani'-JPM 
'Tunaposema yaliyopita si ndwele tugange yajayo sio kwamba tumeyasahau yaliyopita, niwaombe tuendelee kukijenga chama-JPM 
'Zile nafasi za mwenyekiti kuchagua wajumbe wa NEC zimepungua, badala ya 10 nitachagua 7, lengo kutengeneza mwelekeo wa chama kipya'- JPM

'Nawaomba mtembee kifua mbele ninyi ndio watawala, hakuna chama kingine tawala'-JPM 

No comments:

Powered by Blogger.