YANGA WAZIDI KUWATISHA SIMBA
Wachezaji wa Yanga wakimpongeza kiungo Haruna Niyonzima (katikati kulia) baada ya kufunga bao la ushindi dakika ya 52 wakiilaza 2-1 Ruvu Shooting jioni ya leo katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Ruvu Shooting walitangulia kwa bao la Abrahman Mussa dakika ya nane kabla ya Simon Msuva kuisawazishia Yanga dakika ya 32 akimalizia pasi ya Nahodha Niyonzima
Kiungo wa Ruvu, Said Madega (katikati) akipambana na washambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa (kulia) na Amissi Tambwe (kushoto)


No comments: