BAADA YA KUMPIGA JPM MASWALI MWANDISHI PASCAL MAYALLA AWA GUMZO KWENYE MITANDAO YA KIJAMII,WANANCHI WENGI WAMPA PONGEZI

 {MWANDISHI  WA HABARI  BW : PASCAL MAYALA  AMBAYE  AMEZUA GUMZO  KWENYE  MITANDAO  YA  KIJAMII  KUTOKANA  NA  SWALI  KWAKE  KWA  RAIS  MAGUFULI }
Respicius Francis ameandika  ujumbe  huu  kupitia ukurasa wake  wa facebook,

Paschal Mayala (mtangazaji wa kujitegemea) umeitendea haki taaluma yako, umetuwakilisha vyema tuliowengi hapo ikulu ,umeonyesha wewe siyo mwandishi njaa ......mpe neno lolote mwandishi huyu.......


 Augustino Maziku huyu jamaa amejitoa kwenye kundi la waandishi habari uchwara yeye yuko smart kichwani
LikeReply12 hrs
Michael Mkwera Maswali yote mawili yaliyoulizwa na Pascal mayala yalikuwa mazuri, lakini majibu yaliyotolewa yanathibitisha kuwa Rais ni zaidi ya katiba.

Bepari Evodius Rutta He is a really great thinker!

Sam Visram Mtu huru hafungwi na Njaa ya tumbo moja, Mtu huru husukumwa na Roho za wengi. Ahsante sana Brother Mungu azidi kukutia Nguvu leo na kesho

Harry Zingula mkutano waleo ulikuwa unatupa kujua wandish wahabar tunao au vlaza tumepata mmojatu wengine vilaza walienda kushangaaa

George Albert aliuliza swali gani samahani sikuangalia au kusikiliza maana alituhimiza tufanye kazi na bunge likazimwa tufanye kazi

Mustafa Juma SWALI KUHUSU RAIS KUINGILIA MIHIMILI MINGINE
KAMA KUSITISHA SAFARI ZA KITAALUMA NJE,KUPIGA MARUFUKU VYAMA VYA UPINZANI KUFANYA SIASA,KAULIZWA NI KATIBA GANI ILIYOMPA MANDATE HIYO
JIBU ALILOTOA WALA USINIULIXE

Juma Ikunga Hongera yake
Paul Sanga Mtu anaye jitambua siku zote hawezi kuuza fikra zake kwa njaa ya siku moja

Erick Cantona Kajitoa kwa ajili ya tahaluma yake nimemkubali kwakwel

Jasmin John Mwabwanga Hongera kwake kwakweli ila czan kwaswali lile km ataruhusiwa tena kuhudhulia
Pili George Akaze buti huo ndio uwandishi bora

ustafa Juma WENGI NI MA OPPORTUNIST WALIKWENDA KWA AJILI YA KUJIPENDEKEZA ILI WAONWE,
BRAVO PASCAL MAYALLA

Benny Magungu Yupo Vizuri !!

Avith Mireni Hongera saana Mayala nimependa swali lako nimejifunza kitu kupitia ww

Iluabby Raphael Ni mwandishi anae jielewa hakuingia kwenye taalamua hy kwa njaa

Nyamhanga Tino Bairi Nikawaza labda ukiingia tu Ikulu na akili nayo inabadilika! Maana waandishi 
wengi wameuliza maswali mepesi, halfu yanajirudia!! Labda hawakuandaa maswali.

Renatus Tantika Huyu Pascal Mayala nimekua nikimfutilia sana ktk mijadala akiwa na mzee Angalien Mpendu...kiukweli anaelewa nin jamii inataka...na nin kinatakiwa kufanywa na wanahabari kutoa taarifa na kuikosowa serikali..na kuipongeza pia hasa penye mafanikio.

Revo Alexandria Jr. Kitu nilicho jifunza ktk mkutano wa Mhe Rais JPM wahariri wa vyombo vya habari. Takribani masaa 2:45 hivi

1. hakuna mwandishi aliuliza kuhusu *Kilimo, Ufugaji wala Uvuvi* Kwa tathmini yangu ni ishara tosha watu wengi hasa mijini hawana habari na wakulima japo bila wao kuzalisha mijini yumkini hali haiwezi kuwa shwari kamwe. Waandishi wengi wanaelekea kupenda habari za siasa zaidi.

2. Waandishi wengi hutumia muda mwingi sana kuisema serikali haijali michezo nchini, ila cha ajabu leo sijaona swali lolote kwa muheshimiwa kuhusu michezo, nchi hii inyoongoza kwa magazeti ya michezo katika ukanda huu wa maziwa makuu inakosa kabisa kuuliza swali kwa raisi juu ya mipango yake na sera zake kwenye michezo?

3. Hakuna mwandishi aliyeuliza juu ya tetemeko la bukoba na ahadi ya raisi kutembelea bukoba mara baada ya kuhairisha safari ile ya Zambia?

4. Pia nimegundua huu muswada wa habari waandishi wanaupenda sana kuliko tunavyodhani, mda wote waliokuwa na raisi wameshindwa kumuonyesha rais juu ya madhaifu ambao yanatajwa kwenye muswada mliokuwa mkiupigia kelele sana.
mkutano huu na raisi umeonyesha nyinyi waandishi mnapenda sana muswada huo sasa naomba upite haraka ili uanze kazi mara moja.
Asanteni.
Clemence Moshi Safi sana Great thinker

Machunde Mauma Mayalla kauliza maswali mazuri sana. Tatizo hayakujibiwa kabisa. Mazungumzo yalikuwa mengine kabisa nje ya maswali yaliyoulizwa.

Godfrey Jmd Ongera lkn nahisi huyu jamaa alitukanwa ,pale alipo ambiwa jina lake kikwao linamaanisha njaa,kwahiyo swali lake pia limeka kinjaa,namwingine niwa tbc aliyeambiwa ulitaka niseme nakupenda?kiukweli mg aliniudhi kwakahuli hiyo

Kwel kabisa katk wote waliouliza maswali huyu jamaaa ndo kanifurahisha na kanigusa sana....kauliza bila woga.

Brighton Ratinus Hongera kwake aisee lakini nina wasiwasi na usalama wake angefanya mpango akahama kwa mda maana mmh! Akili zao wanazijua 

Adam's Duma Jr. Ameongea kuhusu nn maana nilizima baada ya kuona maswali kama ya school baraza... Nijulishe mkuu wangu


Robert Kyarua Ameitendea haki taaluma yake. Hongera..

Thomas Mwanyelo Na kweli ila jibu la swali lako halijajibiwa kama inavyotakiwa!

Lily Faustin hata mm nilifurahi sana


Gift Ndanshau Yaaani katika waandishi waliyowatendea wtz haki ni mayala tido sami na yule katibu wengine wote ni wachumia tumbo yaani unakuta muhariri mzima anauliza swali la kitoto kbs sijui ni vyeo wameenda kuomba mayala umetutendea haki wtz pamoja na maswali yako hayakupata majibu lkn ujumbe umefika ndiyo sifa ya mwandishi kutokuwa na Njaa Njaa

Rashid Khalifa Kaka tulipofikia kila mtu atapigania maisha kivyake maana mnaendekeza njaa kuliko taaluma yenu mwaka ujao naona mtaitwa mkamwimbie kwaya

Write a reply...


Rose Cyril Well-done Mayala..

Romano Baradyana Umeitetea taaluma yako, hukuweka njaa mbele, hongera 

Mustafa Juma He's not an OPPORTUNIST!!

Rashid Khalifa Kaka tulipofikia kila mtu atapigania maisha kivyake maana mnaendekeza njaa kuliko taaluma yenu mwaka ujao naona mtaitwa mkamwimbie kwaya

Gasto J Mushi Mayala umewadhalilisha wote na hakika wewe ni shujaa hakuna kuogopa wala kuendekeza njaa Tanzanian Hero

Jasmin John Mwabwanga Nitakuombea ckuzote ktk harakati zako labda waje maraika wazuie maombi yangu kwako hongera kwakuonyesha uwezo wako kweli ada yawazazi wako haijaenda bure

Dominick Titus Ameuliza swal ambalo mkuu kaenda chaka kabisa. Hahahaha ngoja wanaoendlea kumuombea waendelee. Mim naendelea kuisoma number

Mustapha Kaponda Kiukweli huyu jamaa naona ndo kama shujaa wa pale magogoni kwa leo.kwani alikua hasemei tumbo lake bali alikua anasemea maslahi ya taifa

Msabila A Fundikira Tatizo ni katiba ipo na inapatikana! Lakini watu wanazungumzia vifungu vifungu tu! Kwa nini hamtumii muda wenu kuisoma katiba yote? Raisi sio mwanasheria hawezi kujaribu kuzungumzia kifungu chochote cha sheria kwa sababu anaweza kukikosea kukitaja halafu ikageuka ndio ajenda kwa wanasheria uchwara kumkosoa raisi! Lakini kifungu alichokitumia raisi ni hiki!

Katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kipengele cha Masharti ya Jumla; Haki na wajibu muhimu Sheria ya 1984 Na 15 ib 6. 29.-(1) Kila mtu katika Jamhuri ya Muungano anayo haki ya kufaidi haki za msingi za binadamu na matokeo ya kila mtu kutekeleza wajibu wake kwa jamii, kama zilivyofafanuliwa katika ibara ya 12 hadi 28 za sehemu hii ya Surah ii katika Katiba.
(2) Kila mtu katika Jamhuri ya Muungano anayohaki ya kupata hifadhi sawa chini ya sheria ya Jamhuri ya Muungano
(3) Raia yeyote wa Jamhuri ya Muungano hatakuwa na haki, hadhi au cheo maalum kwa misingi ya nasaba, jadi au urithi wake.
(4) NI marufuku kwa sheria yeyote kutoa haki, hadhi au cheo maalum kwa raia yeyote wa Jamhuri ya Muungano kwa msingi ya nasaba, jadi au urithi.
(5) Ili watu wote waweze kufaidi uhuru wa binadamu ambavyo misingi yake imeorodheshwa katika Katiba hii kila mtu ana wajibu wa kutenda na kuendesha shughuli zake kwa namna ambayo haitaingilia haki na uhuru wa watu wengine au maslahi ya umma.

Tukiendelea katika kusoma Sheria ya 1984 Na 15 Na 34 ib 6 “Mipaka kwa haki na uhuru na hifadhi kwa haki na wajibu”
30.- (1) Haki na uhuru wa binadamu ambavyo misingi yake imeorodheshwa katika Katiba hii havitatumiwa na mtu mmoja kwa maana ambavyo itasababisha kuingiliwa kati au kukatizwa kwa haki na uhuru wa watu wengine au maslahi ya umma.
(2) Ifahamike kwamba masharti yaliyomo katika Sehemu hii ya Katiba hii, yanayofafanua misingi ya haki, uhuru, na wajibu wa binadamu, hayaharamishi sherio yeyote iliyotungwa wala kuzuia sheria yeyote kutungwa au jambo lolote halali kufanywa kwa mujibu wa sheria hiyo, kwaajili ya –
(a) kuhakikisha kwamba haki na uhuru wa watu wengine au mashali ya umma haviathiriwi na matumizi mabaya ya uhuru na haki za watu binafsi.
(b) kuhakikisha ulinzi, usalam wa jamii, Amani katika jamii, maadili ya jamii, afya ya jamii, mipango ya maendeleo ya miji na vijiji, ukuzaji na matumizi ya madini au ukuzaji na uendelezaji wa mali au maslahi mengineyo yoyoe kwa nia ya kukuza manufaa ya umma;
( c ) kuhakikisha utekelezaji wa hukumu au amri ya mahakama iliyotolewa katika shauri lolote la madai au la jinai.
(d) kulina sifa, haki na uhuru wa watu wengine au maisha binafsi ya watu wanaohusika katika mashauri mahakamani; kuzuia kutoa habari za siri; kutunza heshima; mamlaka na uhuru wa mahakama:
( e ) kuweka vizuizi, kusimamia na kudhibiti uanzishaji, uendeleshaji na shughuli za vyama na mashirika ya watu binafsi nchini; au
(f) kuwezesha jambo jingine lolote kufanyika ambalo linastawisha au kuhifadhi maslahi ya taifa kwa jumla.

(3) Mtu yeyote anayedai kuwa sharti lolote katika Sehemu hii ya Surah ii au katika sheria yoyote inayohusu haki yake au wajibu kwake, limevunjwa, linavunjwa au inaelekea litavunjwa na mtu yeyote popote katika Jamhuri ya Muungano, anweza kufungua shauri katika Mahakama Kuu.
(4) Bila kuhathiri mengineyo yaliyomo katika Katiba hii Mahakama Kuu itakuwa na mamlaka ya kusikiliza kwa mara ya kwanza na kuamua shauri lolote lililoletwa mbele yake kwa kufuata ibara hii; ma Mamlaka ya Nchi yaweza kuweka sheria ajili ya –
(a) kusimamia utaratibu wa kufungua mashauri kwa mujibu wa ibara hii;
(b) kufafanua uwezo wa Mahakama Kuu katika kusikiliza mashauri yaliyofunguliwa chini ya ibara hii;
(c) kuhakikisha utekelezaji bora wa madaraka ya Mahakama Kuu, hifadhi na kutilia nguvu haki, uhuru na wajibu kwa mujibu wa Katiba hii.

(5) Endapo katika shauri lolote inadaiwa kwamba sheria yoyote iliyotungwa au hatua yeyote iliyochukuliwa na Serikali au mamlaka nyingine inafuta au inakatiza haki, uhuru na wajibu muhimu zitokanazo na ibara ya 12 hadi 29 za Katiba hii; na Mahakama Kuu inaridhika kwamba sheria au hatua inayohusika, kwa kiwango inachopingana na Katiba ni batili au kinyume cha Katiba basi Mahakama Kuu ikiona kuwa yafaa au hali au masilahi ya jamii yahitaji hivyo, badala ya kutamka kuwa sheria au hatua hiyo ni batili, itakuwa na uwezo wa kuamua kutoa fursa kwa ajili ya Serikali au mamlaka nyingine yoyote inayohusika kurekebisha hitilafu iliyo katika sheria itakavyotajwa na Mahakama Kuu, na sheria hiyo a hatua inayohusika itaendela kuhesabiwa kuwa ni halali hadi ama marekebisho yatakayofanywa au muda uliowekwa na Mahakama Kuu utakpokwisha, mradi muda mfupi Zaidi ndio uzingatiwe. (Mwisho wa Kunukuu Katika Ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yam waka 1977)
Itaendelea vipengele vingine katika kuwaelimisha Watanzania juu ya vyama vya upinzani katika bunge, haki zao, na mipaka yao kama wapinzani na wakosoaji na warekebishaji wa serikali tawala.

Leonce Swai Aliishia kumjibu kwa zarau tu eti kisukuma Mayala ni njaa,kwa tafsiri ya haraka haraka kaona mayala njaa inamsumbua dah!

Leonce Swai Swali la mwandishi wa kujitegemea Pasco Mayala kwa Magufuli:
Ulitumia mamlaka gani kuamuru Bunge na Mahakama kufanya unayoyataka? Ulitumia mamlaka gani kuzuia mikuatano ya kisiasa
Joseph Lameck Naomba tafadhali munipe kwa ufupi kipande cha elimu Raisi alisamaje kama mulisikiliza kwa makini
Kivuyo Elius Leo ndio nimemuelew huyu jamaa,nimekukubali mkuu

Casmir Dominic Big up kaka mkubwa mayala

No comments:

Powered by Blogger.