Pigo: Rigobert Song apatwa na Kiharusi, yupo hospital na hali yake sio nzuri

Mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Cameroon ambaye pia alikuwa nahodha, Rigobert Song amepatwa na maradhi ya kupooza na amekimbizwa hospitali huko mjini Yaounde, Kameruni. 

Song ambaye amewahi kuvichezea vilabu vya Liverpool na West Ham United amepatwa na hili ikiwa ni ghafla sana. Ikumbukwe pia kuwa huyu ni mjomba wa mchezaji wa zamani wa Arsenal, Barcelona na West Ham United, Alexander Song.

Rigobert Song ambaye pia mpaka anapatwa na maradhi haya alikuwa kocha wa timu ya Taifa ya wakubwa ya Chad, amekumbwa na ugonjwa wa kupooza ambao kitaalamu unafahamika kama cerebral aneurysm, huku pia akisemekana kuwa mahututi sana.

Ulimwengu wa soka upo katika maombi kumwombea mwanasoka huyu wa zamani huku wachezaji kama Patrick Mbona, Samuel Etoo, Jamie Carragher, Stan Collymore pamoja na Robbie Fowler ambao Waliwahi kucheza naye katika ngazi tofauti za vilabu mpaka Timu ya Taifa wakiwa ni watu wa awali kuwahi kutuma salamu za pole na kumwombea kupitia mitandao yao ya kijamii. 


Taarifa zinasema kuwa Rigobert Song ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 40 alipatwa na balaa hili akiwa kwake maeneo jirani ya Ozda, mjini Yaounde.

Rigobert Song aliichezea Liverpool mwaka 1999 akicheza michezo 34 kabla ya kujiunga na West Ham United mwaka 2000. Song pia ndiye mchezaji aliyecheza michezo mingi zaidi akiwa na timu yake ya Taifa baada ya kuichezea kwenye michezo 137. 

Shaffihdauda.co.tz inakuombea hali yako iimarike na urejee katika majukumu yako ya kawaida Rigobert Song. Mungu akuponye.

No comments:

Powered by Blogger.