WANAYANGA MMEMSIKIA HAJI MANARA!
Ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Majimaji umempa kiburi Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Simba Haji Manara na kusema moto wao hauzimiki mpaka mwisho wa msimu.
Manara amesema msimu huu Simba haidharau timu timu yeyote kwenye ligi huku akisisitiza timu yake imejipanga kuongoza ligi kudumu hadi mwisho.
“Macho yetu na masikio yetu tunaelekeza October 1, ni mechi ya kawaida kama mechi nyingine ya ligi na hatuipi u-special wowote ule. U-special wake ni kwasababu ya kucharuana kwa mashabiki lakini uzito ni ulele tulioutoa kwenye mechi ya Majimaji ndio tutautoa ligi nzima hatutadharau timu yeyote”, amesema Manara mara baada ya mechi kati ya Simba dhidi ya Majimaji.
“Tutacheza na Yanga kama tunacheza na mkubwa mwenzetu, hatujali hii ni timu ndogo au kubwa tunatakiwa tuongoze ligi kwa kudumu hadi ligi inamalizika.”
“Hatutadharau mechi inayokuja, mechi ya leo ni sawa na mechi inayokuja bila kujali ni Yanga au timu nyingine yeyeyote, kila mechi ni fainali hiyo ndiyo kaulimbiu ya Simba msimu huu.”
No comments: