Yanga wanaripotiwa kutumia zaidi ya milioni 200 kumsajili Mzambia
June 17 2016 mtandao wa soccer24.com umeripoti habari ambazo huenda zikawa na ukweli kutokana na taarifa hizo kutoka ikiwa ni masaa 11
yamepita toka www.herald.co.zw waliporipoti habari kama hizo na awali tulizichukulia kama tetesi ambazo hazikuwa na nguvu.
Kama iatkuwa kama inavyoripotiwa, hii itakuwa ni good news kwa mashabiki wa Yanga, mitandao hiyo yote imeripoti Yanga kukamilisha usajili wa mzambia Obrey Chirwa kwa ada ya uhamisho wa dola 100000 za kimarekani ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 200.
Obrey Chirwa kama akijiunga na Yanga kama inavyoripotiwa atakuwa kaungana na wachezaji wenzake wa zamani wa FC Platnum Thabani Kamusoko na Donald Ngoma,Yanga wamevutiwa na nyota huyo kutokana na Ngoma na Kamusoko kufanya vizuri katika kikosi cha wakiwa na msimu wa kwanza hivyo wanaimani na Obrey Chirwaambaye anaripotiwa kuwa ataingia Tanzania leo June 17.
No comments: