YANGA ITAWAPIGA ‘BAO’ LINGINE SIMBA KWA TELELA

Salum Telela
Salum Telela ameshindwa kuzungumzia ‘mustakabali’ wake baada ya kumaliza mkataba wake katika klabu ya Yanga SC
. Nahodha huyo wa zamani wa timu za Taifa za vijana na klabu ya Moro United ameshinda mataji mengi katika misimu yake 6 akiwa na timu hiyo iliyomsaini akiwa kinda mwaka 2010 akitokea Moro United.
Nilifanya naye mahojiano mafupi na kikubwa nilitaka kufahamu ni wapi atacheza msimu ujao kufuatia kuwapo kwa habari kuwa anahitajika sana na mahasimu wao Simba SC.
“Nimecheza kwa misimu 6 katika timu hii na nimepata mafanikio makubwa ikiwemo ushindi wa mataji ya ligi kuu (2010/11, 2012/13, 2014/15, 2015/16,) nimeshinda Kagame Cup 2011 na 2012, Ngao ya Jamii 2013, 2014, 2015, pia taji moja la FA.”
“Msimu uliopita kulikuwa na ushindani mkubwa sana lakini niliweza kupambana na kucheza zaidi ya michezo 20. Ukitazama hata uwiano wa mechi kwa wachezaji wa nafasi yangu hazikupishana sana. Nilikuwa na msimu mzuri. Pia nafurahi kufanya kazi na kocha mzuri kama Hans Van der Pluijm na kila mmoja katika benchi la ufundi.”Nilimuuliza, Telela, ni kweli unaondoka Yanga? lakini akajibu kwa namna ya kutohitaji kuzungumzia mambo ya usajili. “Habari hizo naomba tuachane nazo, ni mapema kujadili hayo.”
Telela amekuwa akiwindwa na Simba lakini Yanga wamepanga kukamilisha usajili wake kabla ya kumalizika kwa wiki hii.
Kwa ukaribu zaidi, tafadhali unaweza ku-LIKE PAGE yangu BSports. Utapata Updates za michuano mbalimbali.

No comments:

Powered by Blogger.