Huu mradi wa kitapeli wa IPTL una nguvu ya Nani? soma ufafanuzi wa Zitto hapa

Serikali ya Rais Magufuli kuifadhili IPTL tshs 100 bilioni 2016/17 ?
Nasoma nyaraka za Bajeti naona Serikali imepanga fedha kubadilisha mtambo wa IPTL kwenda kuwa wa Gesi. IPTL ni kampuni binafsi
ambayo inamilikiwa kiutapeli na kampuni ya PAP kufuatia wizi wa fedha za akaunti ya TEGETA Escrow iliyokuwa Benki Kuu. Serikali inayopambana na ufisadi inawezaje kutoa fedha za umma kuwapa kampuni ya kifisadi?Hawa PAP walikuja nchini na briefcase, wakachota fedha BOT wakahonga maafisa wa Serikali, Wabunge, Majaji, Mawaziri na kadhalika. Wakapewa mtambo bure. Wanalipwa kila mwezi tshs mabilioni ya capacity charges. Sasa wanafadhiliwa na Serikali kugeuza mtambo wao kuwa wa Gesi Asilia.
Rais analalamika kila siku nchi kuwa shamba la Bibi. Rais litazame hili la IPTL tafadhali. Kweli Serikali inatenga fedha kuifadhili kampuni hii? Maazimio ya Bunge yanasiginwa namna hii?
Huu mradi wa kitapeli wa IPTL una nguvu ya Nani?
IPTL conversion to Gas sub vote 3198 in vote 58 Ministry of Energy and Minerals. 2014/15 ZERO 2015/16 ZERO and 2016/17 tshs 100bn.
Fedha ya umma kwenda kuifadhili kampuni binafsi ya kitapeli ya IPTL. Tuliambiwa hawa ni wawekezaji ambao watawekeza mpaka kuzalisha 500MW. Leo Serikali inawapangia fedha ya Bajeti.
IPTL mradi wa Nani?
IPTL mradi wa Nani?

No comments: