Chadema kuwafungulia polisi kesi

Kahama. Chadema kimesema leo kinatarajia kufungua kesi Mahakama Kuu kanda ya Mwanza dhidi ya Polisi, kupinga zuio la maandamano mikutano ya hadhara
ya kisiasa.
Akizungumza mjini Kahama jana, Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe alisema mikutano ya hadhara ni haki ya kikatiba na hawatanyamaza inapozuiwa na mtu, au mamlaka yoyote.
“Tutapambana kwa njia na nguvu zote kulinda demokrasia nchini, hata kama itabidi kufia uwanjani. Ikibidi kwenda mahakamani kudai haki hiyo tutafanya hivyo.” alisema
Hata hivyo, Mbowe hakuwa tayari kuthibitisha taarifa za Chadema kufungua kesi jijini Mwanza, leo.
Mawakili wa Chadema akiwamo Peter Kibatala na Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu walitarajiwa kuwasili Mwanza jana tayari kutoa ushauri wa kisheria na kufungua kesi
No comments: