MWADUI YAPELEKA JANGWANI KOMBE LA VPL

DSC_0059
Kocha wa Mwadui FC ametangaza kuikabidhi rasmi Yanga kombe la VPL baada ya kuichapa Simba kwa bao 1-0
kwenye mchezo wa ligi kuu uliochezwa kwenye uwanja wa taifa jioni ya leo.
DSC_0024
DSC_0024
Simba watajilaumu kwa kupoteza nafasi nyingi za kufunga walizozipata kwenye mchezo kabla ya kubanwa na kutunguliwa bao katika dakika za lala salama.
DSC_0012
Jamal Mnyate ndiye shujaa kwa upande wa Mwadui kutokana na kupachika bao pekee katika mchezo huo na kuihakikishia timu ya Mwadui ushindi wa ugenini.
DSC_0013
Licha ya kufanya mabadiliko ya kuwaingiza Ibrahim Ajib, Brian Majwega na Musa Hassan ‘Mgosi’ bado haikusaidia kutamba mbele ya wachimba madini ya Almasi kutoka mkoani Shinyanga wakiwa chini ya kocha wa zamani wa Simba Jamhuri Kihwelo.
Simba ikiwa na wachezaji wake wa kulipwa Vicent Agban, Emery Nimubona, Juuko Murshid, Justice Majabvi na Hamisi Kiiza, ilitulizwa na nyota wa Julio ambao wengi ni wakongwe waliotamba kwenye ligi ya Vodacom na timu mbalimbali.
DSC_0026
Mambo muhimu kufahamu
  • Mchezo wa kwanza Mwadui ikiwa mwenyeji wa Simba kwenye uwanja wa CCM Kambarage timu hizi zilitoka sare ya kufungana bao 1-1, ilikuwa December 26, 2015.
  • Mara ya mwisho Simba kushinda kwenye mchezo wa ligi ilikuwa March 19, 2016 ilipoifunga Coastal Union magoli 2-0 kwenye uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
  • Simba haijapata ushindi tangu ilipofungwa na Coastal Union kwa magoli 2-1 kwenye mchezo wa nusu fainali ya kombe la Azam Sports Federation Cup.
  • Hii ni mara ya tatu Simba inacheza dhidi ya Mwadu, mechi mbili zikiwa ni za ligi mechi moja ya kirafiki ya kujipima nguvu iliyochezwa kabla ya kuanza kwa msimu huu wa ligi na timu hizo kutoka suluhu (0-0)
  • Simba ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 58 baada ya kucheza mechi 27 za ligi huku ikiwa imebakiza michezo mitatu ili ligi kumalizka.
  • Mwadui imebakiza mechi mbili kuhitimisha michezo yake ya ligi, ipo katika nafasi ya sita ikiwa na jumla ya pointi 40 baada ya kushinda mchezo dhidi ya Simba.
  • Katika mechi 27 ambazo Simba imecheza, imepata ushindi kwenye mechi 18, imetoka sare mara 4 na kupoteza michezo 5 huku ikiwa imefunga magoli 43 na kuruhusu nyavu zake kutikiswa mara 15 hivyo inatofauti ya magoli 28
  • Mwadui imejipatia ushindi mechi 11, sare 7 na kupoteza mechi 10 kati ya mechi 28 ilizocheza. Imefunga magoli 28 na kufungwa magoli 26, inaofauti ya magoli mawili ya kufunga na kufungwa.

No comments:

Powered by Blogger.