Umpe Nini Mpenzi Wako Asikuache?


Ni moja ya swali muhimu ambalo huulizwa na watu wengi waliopo katika mahusiano, wakiwa na lengo la kutaka kujua mahitaji sahihi ya wapenzi
wao kwa kuhofia kuachwa. Wanawake wanahitaji mambo matano muhimu ambao ni haya:
Kwanza wanawake wanataka kutatuliwa matatizo yao.
Wengi hutegemea kuwa wanapokuwa na wapenzi watasaidiwa katika matatizo ya kimaisha na migogoro ya kimawazo. Kwa mfano ushauri juu ya maisha yao, kulindwa na hatari za kimaisha.
Jambo la pili wanalohitaji wanawake wengi ni kubembelezwa.
Wanawake hupenda kubembelezwa pale wanapokuwa na huzuni, wengi wao hawapendi kukaripiwa, mara nyingi hupenda kuungwa mkono wanapokuwa na misuguano na wengine. Ili mwanaume amteke kimapenzi mwanamke lazima awe nyuma yake hata kama atakuwa na kosa. Wanawake wengi hupenda kuelimishwa zaidi kuliko kufokewa.
La tatu muhimu kwa mwanamke ni kumuweka namba moja.
Safari ya penzi la mwanamke haishii kwenye kumpata na kumliki, kisha kujisahau kwa kisingizio kuwa umemuoa au umemvisha pete ya uchumba, ni zaidi ya hapo. Jambo la tatu ambalo wanawake wengi huhitaji ni kuwa namba moja au kupewa kipaumbele.
Jambo la nne ni kulidhiswa katika tendo la ndoa.
Hata kama utakuwa na kiwango kikubwa cha mapenzi juu ya mpenzi wako kwa kiwango gani, ukiwa dhaifu katika tendo la ndoa utayumbisha penzi lako. Ni wajibu wa mwanaume kuhakikisha kuwa anamtosheleza mpenzi wake katika tendo hilo. Utundu unahitajika ili kumkata kiu mpenzi wako.
MAALUM: Umuhimu wa Kujifunza Saikolojia
La mwisho ni kumpa uhuru wa kuzungumza au kueleza hisia zake.
Wanawake wanatajwa kuzungumza maneno 25,000 kwa siku, huku wanaume wakibaki na kiwango cha maneno 5,000 kwa siku, hii ikiwa na maana kuwa wanawake hupenda zaidi kujieleza walivyo mbele ya wengine. Kwa msingi huo wakizuiwa wasiongee hujiona kama wanakosa nafasi muhimu.

No comments:

Powered by Blogger.