Upigaji kura Uganda wayumba
WAPIGA kura nchini Uganda
wanaendelea
kupiga kura vituoni kuwachagua viongozi lakini katika baadhi ya vituo upigaji
kura umeyumba kutokana na kuchelewa kuanza.
Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) limeripoti kwamba, hali
hiyo imetokana na vifaa na karatasi za kupigia kura kutofikishwa vituo kwa
wakati katika baadhi ya maeneo.
Mjini Kampala
ambapo ni Makao Makuu ya Tume ya Uchaguzi nchini humo, bado kuna vituo ambavyo
kufikia saa nne upigaji kura haukuwa umeanza.
Hata hivyo, tume
hiyo kwenye ukurasa wake wa Twitter, imeandika: “Tunabaki kuwa na matumaini na
tunawahikishia kwamba nyote mtaweza kupiga kura leo. Tunasikitika kutokana na
kuchelewa huku. Asanteni.”
Kuhusu iwapo
muda wa kupiga kura utaongezwa, tume hiyo kupitia mitandao ya kijamii imesema
kwa mujibu wa sheria, ni sharti vituo vifungwe saa kumi alasiri.
Tume hiyo
imeahidi kuhakikisha wapiga kura wote watakaojitokeza kufikia wakati huo
wanapiga kura
No comments: