Umeisoma ya Wema kumpongeza Diamond Baada ya kutwaa tuzo 3, amuita ‘kaka’, Zari achukua nafasi yake rasmi!!!

 

It’s official, Diamond na Wema Sepetu hawapo pamoja tena. 

Habari hiyo imekuja katika siku ambayp Diamond

amegeuka shujaa kwa kunyakua tuzo za tatu za Channel O.
Miongoni mwa watu waliompongeza kwa ushindi huo ni Wema Sepetu ambaye tumezoea akimuita staa huyo ‘my baby’, awamu hii ameitwa ‘kaka’.

“Gnyt Instagramers… And Hongera tele ziende kwa kaka platnumz… I must say he did Tanzania proud,” aliandika Wema kwenye Instagram muda mfupi baada ya tuzo hizo kuisha ikimaanisha kuwa alikuwa akizifuatilia.


Tofauti na kwenye tuzo za MTV MAMA, msichana aliyekuwa ubavuni mwa Diamond kwenye tuzo hizo ni Zari the BossLady – na hivyo kuthibitisha tetesi zilizovuma kuwa wawili hao ni wapenzi.

Pamoja na Zari, Diamond alisindikizwa na mama yake ambapo walikuwa pamoja na Zari kwenye red carpet na hata kuzunguka pamoja jijini Johannesburg.

No comments:

Powered by Blogger.