Picha ya Roma na mdogo wa kike wa Ali Kiba ilivyozua utata,imekuaje?
Ikiwa zimesalia wiki kadhaa
ili msanii wa
Hip Hop Tanzania,Roma kufunga ndoa na mpenzi wake anayejulikana
kama Nancy au Mama Ivan kumeibuka na utata baada ya kusambaa kwa picha ya
msanii huyo akiwa kwenye pozi linaloonekana ni la kimahaba na zabibu Kiba,mdogo
wa kike wa Ali Kiba na watu kuhisi huenda wawili hao wakawa wana mahusiano ya
kimapenzi
Kituo cha redio kimoja
kilimtafuta mke mtarajiwa wa Roma na kumuuliza kuhusiana na picha hiyo ambapo
bibie huyo alidai kuwa hajui chochote na wala hajali kwani inaweza ikawa picha
tu na shabiki na kuongeza kuwa Roma hawezi kufanya upuuzi.
Kwa upande wake Roma
alipotafutwa alionekana mwenye kusita sita na kutaka kujua kama mazungumzo hayo
yapo On air au Off Air,baadaye Roma alikiri kuwepo kwa picha hiyo na kudai ni
ya kitambo na hakumbuki ilikuaje kwenye picha hiyo na kuomba aulizwe zaidi
kuhusiana na kazi za muziki kuliko mambo mengine ya nje.
Source: Clouds
No comments: