Kwa mara ya kwanza Jose Mourinho kavunja ukimya kuhusu stori za yeye kurudi katika soka



 Baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu kwa kocha wa zamani wa klabu ya Chelsea Jose Mourinho, February 7 karudi kwenye headlines na kauli mpya baada ya kutokuwa tayari kuzungumzia soka, Jose Mourinho ameamua kuzungumzia soka ikiwa ni wiki sita zimepita toka afukuzwe kazi na Chelsea.
Jose Mourinho ambaye amekuwa akihusishwa kujiunga na Man United ili arithi nafasi ya Louis van Gaal alikuwa hayupo tayari kuzungumzia soka, ila kwa sasa amekubali kulizungumzia hilo na kukiri kuwa yupo karibu kurudi kazini hivi karibuni, licha ya kuwa wengine huwa wanamtafsiri kama jeuri, lakini yeye anasema ni mtu wa kawaida na anajifunza popote.
30EE955400000578-0-image-a-39_1454801333785

No comments:

Powered by Blogger.