Harry Redknapp "Jose Morinho ameshakubali kuchukua kibarua United"


Tetesi zilizoanza kuenea tokea January huenda zikawa kweli
kwani katika mahojiano na Radio moja jijini london Harry Redknapp amesema Jose tayari ni kocha wa Man United. Redknapp ni mmoja kati ya makocha wanaoheshimika uingereza kwakufanya kazi nzuri akiongoza club kama QPR na Totenham Spurs ambayo aliifikisha robo fainali Ligi ya mabingwa ulaya (uefa) kimpindi cha nyima. Harry Redknapp aliendelea kusema kuwa Luis Van Gaal amekosa utashi na mbinu zake au ufundishaji wake hauendani na club ya Manchester United.

Hivi karibuni mambo yamezidi kuwa mabaya kwa Luis kwani timu yake imekuwa ikipoteza michezo iliyotegemewa kuwa ni mirahisi kwa timu kama Manchester Unided. Kipigo dhidi ya Sunderland weekend iliyopita kimewakera sana mashabiki wa united na pia wamiliki wa Manchester United wameona ni vema Jose Morhino achukue mikoba ya Van Gaal


No comments:

Powered by Blogger.