Fedha za CCM zavuruga vyama Z’bar
FEDHA za Chama Cha Mapinduzi (CCM)
zinatumika kuvuruga mwelekeo na msimamo wa vyama vya upinzani visiwani
Zanzibar, anaandika Regina Mkonde.
Kazi hiyo inafanywa kwa ustadi mkubwa na maofisa wa CCM visiwani
humo kwa kushirikiana na maofisa wa Bara ili kuhakikisha Tume ya Uchaguzi
Zanzibar (ZEC) inapata uhalali wa kuendesha uchaguzi huo ambao umegubikwa na
utata wa kikatiba na hata kugomewa na vyama, taasisi na wanataaluma nchini.
Fedha hizo
zinachomekwa katika vyama ambavyo vinaonekana kutokuwa na msimamo wa pamoja
ambapo Chama Cha National Reconstruction Alliance (NRA) pamoja na Chama cha
Alliance for Democratic Change (ADC) vimekumbwa na mtikisiko wa fedha hizo.
Tayari vyama 10 vimejinasua kwenye mtego huo.
Wakati Said
Miraji, Mwenyekiti wa ADC akienda mbio kuokoa dhoruba ya fedha za CCM kuvuruga
msimamo wa chama hicho wa kutoshiriki uchaguzi Zanzibar, kauli tata zimeendelea
kuibuka ndani ya NRA.
Ni siku mbili
zimepita baada ya aliyekuwa mgombea urais wa NRA, Seif Ali Iddi aliyeongozana
na Suleiman Mohamed Gaddafi, Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho kutoa tamko la
kutoshiriki kwenye uchaguzi huo, baadhi ya viongozi wa NRA leo wameibuka na
kukanusha tamko hilo kwa kudai “ni tamko la mgombea na si la chama.’
Akizungumza na
waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa Maelezo jijini Dar es Salaam, Hassan
Kisabya Almas, Katibu Mkuu-Bara na bodi ya chama hicho wameeleza kwamba, tamko
la mgombea wao halina baraka zao.
“Kujitoa kwake
kwetu si hoja, lakini sifa zote hizo haziwezi kukitoa chama katika jambo lolote
ikiwa chama kimeamua,” amesema Almasi huku akiongeza kuwa, watajiaminisha kuwa
mgombea wao ama amehama chama au amefariki.
MwanaHalisi
Online ilimtafuta mgombea huyo (Iddi) na kumuuliza juu ya tuhuma za baadhi ya
viongozi wa chama chake kutokana na kutangaza kujitoa kwenye uchaguzi huo
uliotangazwa kufanyika tarehe 20 Machi mwaka huu.
Iddi amejibu,
“tulikaa kikao tarehe 6 Januari mwaka huu na mwenyekiti wa chama na katibu
tukaafikiana kutoshiriki kwenye uchaguzi wa marudio, viongozi wa bodi
waliojitokeza leo wamenunuliwa,” amesema.
Iddi amesema
kuwa, yeye binafsi hakukubali kushiriki kwa sababu, ufutwaji na urudiwaji wa
uchaguzi huo haukuzingatia sheria na katiba, huku akimtaja ofisa mmoja wa ngazi
ya juu katika Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini kuhusika na harakati
za kurubuni vyama vya siasa kwa maslahi ya CCM.
“Huyu (anamtaja
jina) anahusika kuvirubuni vyama kwa masilahi yake binafsi, na hawa viongozi
waliojitokeza leo hawana msimamo,” amesema Iddi.
Chama cha NRA ni
miongozi mwa vyama 14 vilivyosimamisha wagombea katika uchaguzi wa Tarehe 25
Oktoba mwaka jana kwa nafasi ya Rais ambapo ZEC ilifuta uchaguzi huo siku tatu
ba
chanzo:Mwananchionline
No comments: