LIVERPOOL YAPATA POINTI 3 UGENINI, LAKINI YAKIONA CHA MOTO

Lalana
Adam Lalana amewatoa Liverpool kimasomaso baada ya kuifungia timu hiyo bao la ushindi dakika za lala salama kwenye mechi
ya ligi kuu England kati ya Norwich City dhidi ya Liverpool iliyomalizika kwa magoli tisa (9) kufungwa kwenye game hiyo.
Lalana 5
Roberto Firmino alianza kuweka kambani bao la kwanza kuiweka Liverpool mbele ya Norwich kabla ya Dieumerci Mbokani kuisawazishia Norwich kwa bao la kisigino.
Lalana 3
Steven Naismith akapachika bao la pili na kuifanya Norwich kuongoza kwa bao 2-1 hadi mapumziko.
Lalana 4
Wes Hoolahan akaongeza goli la tatu kwa mkwaju wa panati upande wa Norwich dakika chache baada ya kuanza kwa kipindi cha pili kabla ya Jordan Henderson na Firmino kupiga mabao na kuufanya mchezo huo kuwa sawa kwa magoli 3-3.
Lalana 2
James Milner akatupia bao jingine na kuifanya Liverpool kuwa mbele kwa bao 4-3. Sebastian Bassong aliifungia Norwich bao la kusawazisha zikiwa ni dakika za nyongeza lakini bao hilo halikudumu baada ya Lalana kuipa Liverpool ushindi wa ugenini kwa kufunga bao la tano na kufanya matokeo yasomeke Norwich 4-5 Liverpool

No comments:

Powered by Blogger.