BREAKING NEWS: NI JPM TENA ALITIKISA TAIFA DUNIA YASIMAMA KUSHANGAA TUKIO ALILOFANYA MAWAZIRI WAKE WAMLILIA..
Tangu alipoingia madarakani mwaka mmoja uliopita, Rais John Magufuli amekuwa akifanya mambo kadhaa ambayo yamekuwa yakitikisa ndani na nje ya nchi kubwa likiwa ni staili yake ya kubana matumizi na kurejesha nidhamu kwa kada zote za utumishi wa umma.
Katikati ya wiki, Rais Magufuli aliibuka na kishindo kingine ambacho wadadisi wa mambo wamekielezea kuwa ni ujumbe tosha kwa mawaziri wake na viongozi wengine waandamizi wa Serikali. Mkewe, Janeth Magufuli alilazwa kwa siku mbili katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) baada ya kuugua ghafla na kupoteza fahamu.
Janeth alilazwa Novemba 9 na kuruhusiwa kutoka Novemba 11 kwa ugonjwa ambao haukutajwa, zaidi ya kuelezwa kuwa alikuwa amepoteza fahamu wakati akifikishwa hospitali hiyo kubwa zaidi nchini.
Alilazwa jengo la Sewahaji ambalo lina wodi za kawaida, za kati na za watu mashuhuri ambazo ni vyumba vya mgonjwa mmoja vyenye huduma binafsi kama vyoo na bafu. Pia, katika kuonyesha kuwa hakuna mipango ya kumpeleka nje kwa matibabu zaidi, taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais ilimkariri mke huyo wa Rais akisema, “Nipo vizuri na madaktari wameniruhusu nirudi nyumbani ambako nitamalizia matibabu yangu”.
Watu waliofuatwa na Mwananchi kutoa maoni yao kuhusu suala hilo, walisema inawezekana ni moja ya mikakati ya Rais Magufuli kutaka wananchi wawe na imani na hospitali za ndani na pia suala la kubana matumizi, lakini ni salamu kwa viongozi.
“Watu hatujazoea kuona viongozi wa kitaifa wakitibiwa hospitali za ndani licha ya kwamba Muhimbili ni hospitali kubwa ya kimataifa yenye wataalamu wengi na wabobezi katika huduma wanazozitoa,” alisema Profesa Gaudence Mpangala wa Chuo Kikuu cha Ruaha.
Aliongeza kuwa kitendo hicho kinaonyesha imani ya Rais kwa huduma za afya zinazotolewa na inapunguza tabaka la maskini na tajiri katika upatikanaji wa huduma hiyo.
Alisema pia uamuzi huo wa mke wa Rais kutibiwa hospitali za ndani ya nchi kimeokoa fedha nyingi kwa kuwa angetibiwa kwa gharama kubwa huku wasaidizi wake wakilazimika kusafiri naye.
Profesa Mpangala alisema uamuzi huo utasababisha huduma katika hospitali za ndani kuboreshwa kwa kuwa viongozi watakapokuwa wakitibiwa, watabaini upungufu na kuufanyia kazi.
Hoja hiyo inafanana na ya Profesa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Benson Bana ambaye alisema Rais Magufuli ameonyesha kuwa na imani na taasisi zake, akisema kitendo hicho ni somo kwa viongozi walio chini yake kutofuata matibabu nje ya nchini wakati yanaweza kupatikana nchini.
“Nadhani viongozi wa chini yake sasa watajifunza kuwa na imani na huduma za nyumbani. Rais Magufuli ameiamini Hospitali ya Taifa analoliongoza. Siyo unakuta waziri wa elimu anaenda kumsomesha mtoto wake nje ya nchi, tafsiri ya kufanya hivyo ni kwamba hana imani na kile anachokisimamia,” alisema Profesa Bana.
Mkazi wa Kijitonyama, Dadley Jackson alisema Rais anapaswa kupongezwa kwa uamuzi huo kwa kuwa si rahisi viongozi wa mataifa ya Afrika au familia zao kulazwa hospitali za ndani ya nchi wanazoziongoza.
“Viongozi wengine wanatakiwa kuiga mfano wa kiongozi huyo kwa kupata matibabu yanayowezekana katika hospitali za ndani, huku Serikali ikiwekeza nguvu zaidi katika sekta ya afya ili huduma zote muhimu ziweze kupatikana ndani na zisifuatwe tena nchi za watu,” alisema Jackson.
Mkurugenzi Mkuu wa MNH, Profesa Lawrence Museru alisema Mama Magufuli alipokewa hospitali hapo kama wagonjwa wengine na madaktari waliposhauri alazwe, Ikulu ilikubali licha ya kwamba kulikuwa na uwezakano wa kupelekwa hospitali nyingine kubwa.
“Kwa namna fulani, Rais na Ikulu kwa ujumla wameonyesha kuwa na imani na huduma zinazotolewa na Hospitali ya Taifa kwa kuwa walikuwa na uwezo wa kumpeleka hospitali nyingine ambayo wangedhani ni bora zaidi,” alisema Profesa Museru.
Tangu aingie madarakani, Rais Magufuli amekuwa akisisitiza kudhibiti matumizi yasiyo na lazima, ikiwamo safari za nje ya nchi, za ndani, ukubwa wa misafara ya viongozi na matumizi ya fedha nyingi kwenye sherehe za kitaifa.
Ameonyesha njia kwa yeye mwenyewe kutosafiri mara kwa mara nje ya nchi, ambako hadi sasa ametoka mara tatu licha ya kupata mialiko 47 na mara kadhaa katika safari zake za mikoani hutumia barabara. Pia amefuta sherehe za kitaifa na kuagiza fedha zilizotengwa kwa ajili ya shughuli hizo, zielekezwe kwenye miradi ya maendeleo.
Hivi karibuni, alipunguza idadi ya wageni walioalikwa sherehe za kuzima Mwenge wa Uhuru mkoani Simiyu
No comments: